Saturday, August 17

MABALOZI WALIOAPISHWA JANA WAMUAGA MAKAMU WA RAIS LEO – Full Shangwe Blog

0


1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa, Balozi Slaa alifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga akiwa tayari kuelekea kwenye kituo chake kipya cha kazi.

2

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto aliyefika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo kipya cha kazi, katikati ni Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

3

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.

5

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

………………

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria  Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wakutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

 

Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Ikulu jijini Dar Es Salaam .

 

Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji  ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.

 

Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais  kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.