Thursday, August 22

DR.GEODAVE KISAMBALE :WATANZANIA DUMISHENI AMANI MLIOPEWA

0


IMG-20190423-WA0022

Picha ikionyesha Nabii Dr Geodave kisambale akihudumia waumini wake .

…………………

Na Woinde Shizza  , Arusha  

Watanzania wametakiwa kudumisha amani na upendo  uliopo  katika nchi yetu kwani ndio zawadi  pekee tulioachiwa na mwenyezi mungu.

Hayo yamebainishwa na nabii mkuu Wa kanisa la Ngurumo ya upako Dr  Geordave  Kisambale jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha unabii iliofanyika kosongo jiji hapa.  

Alisema kuwa watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na mungu ivyo niwajibu Wa kila MTU kuienzi ,kuidumisha   pamoja na kuilinda.

“Unajua mungu anatupendelea sana Watanzania ametupa amani ya nchi yetu ,ametufanya tunaishi kwa upendo angalieni nchi zingine wanapigana kila siku ,kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani   lakini sisi watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu” alisema Geodave

Aidha aliwataka watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi mungu.

Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea  nchi yetu ya Tanzania iendelee  kuwa na amani pia aliwakumbusha kuwaeka viongozi wetu Wa kitaifa akiwepo Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.

Aidha amewataka watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza Chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.

Share.

About Author

Leave A Reply