Thursday, February 21

DKT. JINGU AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

0


Pix 1

Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza na Watumishi wa Idara Kuu hiyo katika ukumbi wa Chuo Kikuu Dodoma kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo.

………………………..

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

 Na Mwandishi wetu Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. John Jingu amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kutofanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu katika kuleta ufanisi katika utendaji kazi wao ili Wizara iweze kutimiza malengo yake.

Amesema hayo wakati wa kikao kazi  na watumishi wa Wizara yake kwa lengo la kujitambulisha lakini pia kusikiliza mawazo ya watumishi wake kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Dkt. Jingu amewataka wafanyakazi hao kuongeza ubunifu lakini pia amehaidi kuboresha mazingira ya kufanyia kazi akilitaja jambo hilo kuwa suala la kipaumbele ili wafanyakazi waweze kutekeleza kazi kwa ufanisi zaidi na kuisaidia serikali kufikia malengo tarajiwa.

Ameongeza kuwa anashughulikia changamoto ya Vitendea kazi kwa watumishi kama vile kompyuta, magari na vifaa vingine kwa kuwa katika upitaji wake katika ofisi za watumishi amebaini watumishi wana mapungufu ya vitendea kazi jambo linalopunguza ufanisi wa kazi.

‘’Mtu hasishindwe kufanya kazi kwasababu ya kukosa vitendea kazi sisi viongozi tutajitahidi kuleta vitendea kazi vyote ili kuboresha utendaji kazi katika wa wizara yetu na kwasasa tunatarajia kuongeza idadi ya vitendea kazi ’’.Aliongeza Dkt. Jingu

Aidha Dkt. Jingu amesema kwa muda mfupi aliokaa na watumishi wake ameona baadhi ya watumishi wanafanya kazi mda mrefu na kuhaidi kuangalia suala la malipo ya kazi za ziada lakini akitahadhalisha kuwa wafanyakazi wazembe wasitarajie kupata malipo hayo.

“Atakayefanya kazi zaidi atapata kingi zaidi na atakayefanya kazi kidogo atapata kidogo zaidi tutao motisha ili wafanyakazi wene bidii wasikate tamaa’’.Aliongeza Dkt. Jingu.

Amewataka Wakuu wa Idara na vitengo kuacha tabia ya kutowapangia kazi wafanyakazi ambao wao wanadhani hawajui kazi kama wanashindwa kuwatumia wawarudishi kwa mahafisa rasilimali watu ili waweze kujua la kufanya kwa watumishi hao.

Aidha Dkt. John Jingu ametaka kuwepo kwa ushirikishwaji miongoni mwa Idara na Idara lakini na watumishi ndani ya idara ili kujenga Jamii ya Wafanyakazi wenye ufanisi kwa manufaa ya Taifa hili.

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply