Saturday, August 17

DC MSHAMA AWAASA MADEREVA BODA KULIPIA VITAMBULISHO VYA UJASIRIAMALI

0


IMG-20190411-WA0008AAA

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ,amewaasa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda ,kulipia vitambulisho vya wajasiriamali na endapo watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria.

 

Aliyasema hayo mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na madereva hao na kusema ,wao ni moja ya kundi ambalo linapaswa kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ambapo wanatakiwa kulipia shilingi 20,000.

Mshama alisema kuwa agizo la watu wanaofanyabiashara ambayo mtaji wake hauzidi kiasi cha sh.milioni nne wanapaswa kuwa na vitambulisho hivyo .

“Mnapaswa kununua vitambulisho hivyo na kwa wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo hivyo hakuna budi kila mmoja wetu kuhakikisha analipia kiasi hicho ili waweze kufanya kazi bila ya usumbufu,” alisema Mshama.

 

Aliwataka wafanyabiashara wengine nao kulipa ili wapatiwe vitambulisho ambavyo Rais ametaka wajasiriamali wadogo wawe navyo kwani nao wanachangia uchumi wa taifa.

 

 

 

“Tunaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wachangamkie fursa hiyo kwani ushuru waliokuwa wakilipa kwa sasa utakuwa haupo na kitambulisho hicho ndicho kitakuwa kimefidia na haitaruhusiwa kufanya bishara kama hawana vitambulisho hivyo,” alisema Mshama.

 

Kwa upande wake Bakari Kapera wa kitengo cha elimu ya mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Pwani alisema kuwa  fedha wanazolipia leseni siyo kodi bali ni ada ili mtu kutambulika kuwa ni dereva.

 

 Stanley Ndunguru kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga na Majini (SUMATRA) alisema kuwa malipo hayo yanalipwa na mmiliki wa chombo na siyo wao kama madereva kwani hawaruhusiwi kulipa ikiwa ni pamoja na bima. 

 

 

 

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Jenifa Omolo alisema kuwa waendesha boda boda nao wametajwa kuwa nao ni mwiongoni mwa wanaotakiwa kulipia vitambulisho hivyo.

 

 

 

Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Pikipiki wilaya ya Kibaha (CHAWAMAPIKI) Shaban Kambi alisema kuwa kilichosababisha wakashindwa kuchukua vitambulisho hivyo ni kutopatiwa elimu juu ya wanaopaswa kulipia.

Share.

About Author

Leave A Reply