Friday, July 19

DC KATAMBI:FEDHA ZA RUSHWA PELEKENI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

0


8a6ecfe7-1bfb-4314-81ea-46f0527e7dde

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amewataka Watanzania kutenga fedha kwa ajili ya kuchangia katika miradi mbalimbali ya mendeleo na si kutenga fedha hizo kwa ajili ya kutoa rushwa ambayo ni kinyume cha sheria.

Katambi aliyasema hayo, wakati akipokea madawati ya shule 40 yenye thamani ya sh, 5.8 million yaliyotolewa na kampuni ya GP 88 Petrol Station.

Amesema kuwa wapo watu ambao wamezoea kutoa rushwa katika taasisi zao hivyo ni vyema fedha hizo wakazitumia kuunga mkono juhudi za Serikali za utoaji wa elimu bila malipo.

“Wapo watu ambao ni watoa rushwa, bila woga wowote, huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, sasa niwape mbinu fedha hizo zitumie kwenye miradi ambayo ni halali,iliyopewa baraka na Serikali ,” amesema Katambi.

Hata hivyo Katambi amesema katika Wilaya ya Dodoma kuna shule 17 zinazoendelea na ujenzi wa madarasa kati ya matatu hadi manne, hivyo bado juhudi za wadau zinahitajika katika kumaliza changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madawati kwa shule hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, hadi ifikapo mwezi juni 2019 jiji litakuwa limefikia asilimia 90 ya ungezi wamaabara zenye hadhi ya Kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Halleluya Kessy amesema ameamua kutoa mchango huo wa madawati ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk, John Magufuli katika sekta ya elimu.

Yusuph Nkuse mwanafunzi wa shule ya msingi Dodoma Makulu amesema kutokana na shule nyingi za vijijini kukabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo wadau wanatakiwa kuziangalia shule hizo na si kuishia mjini tu.

Share.

About Author

Leave A Reply