Friday, July 19

Citibank,Tamfi Wazindua Tuzo Ya Ujasiriamali

0


 

Na Mwandishi Wetu

Mtendaji mkuu Citi bank Tanzania joseph Carasso akizungumza. Mwingine ni wmenyekiti wa bodi ya Tamsi Joel Mwakitalu

Kwa mara ya tatu
mfululizo, CITI Foundation ikishirikiana na Shirikisho la Asasi zinazotoa
huduma ndogo za fedha (TAMFI), jana wamezindua awamu ya tatu ya tuzo za
wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA).

Tuzo hizi
zinalenga kutambua mchango mkubwa wa wajasiriamali kwenye kuinua uchumi wa
familia zao na jamii zinazowazunguka.

Kwa mujibu wa
Mtendaji Mkuu wa Citibank Tanzania, Bw. Joseph Carasso, tuzo za CITI
zimeshamiri na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikio makubwa
kwa wajasiriamali wadogo na walio wabunifu.

Washiriki katika uzinduzi

 

 

Watu walionufaika katika msimu uliopita wakizungumza umuhimu wa tuzo hizo

 

Mtendaji huyo
alisema CITI inaamini kuwa wajasiriamali wadogo wenye ubunifu ndio
wajasiriamali wakubwa wa kesho. Tunawathamini sana.

Tuzo za
wajasiriamali za CITI (CMA) zimekuwa alama kubwa ya utendaji wa kazi za Citi
Foundation kwa zaidi ya muongo mmoja.

Tangu mwaka 2005, wakati
zilipoanzishwa nchini Marekani tuzo za CITI, zimelenga kuleta mageuzi ya
kiuchumi na fursa kwa wajasiriamali katika nchi zaidi ya nchi thelatini duniani
kote.

Hapa nchini katika
awam,u ya tatu , CITI itatoa zaidi ya shilingi milioni 70 kwa washindi kumi na
sita. Na tuzo hizi zitaweka alama na kutoa motisha kwa wajasiriamali na asasi
zinazotoa huduma ndogo za fedha.

waandishi wa habaria wakirekodi tukio

 

Mtendaji wa TAMFI Terry akielezea hafla  ya uzinduzi wa tuzo

 

 

waandishi kazini

 

Washiriki wakibadilkishana mawazo baada ya uzinduzi

 

Malengo ya Citi
Foundation ni kufanikisha kuainisha huduma za fedha jumuishi na kuchangia
Maendeleo endelevu  (Sustainable Development
Goal (SDG) 8,), ambayo pamoja na mambo mengine yanaainisha ajira zenye staha kwa
wote

 Akielezea zaidi, Bw Carasso, alisema kwamba
tuzo hizi pamoja na kuinua viwango vya huduma za fedha jumuishi nchini zinasaidia
mjasiriamali mmoja mmoja kuinua viwango vya maisha vya familia zao na jamii zinazowazunguka
na Taifa kwa ujumla.

Hii inalenga moja
kwa moja malengo ya SDG 9.3 ambalo linalenga kuongeza  idadi ya wajasiriamali wadogo katika nchi
zinazoendelea pamoja na huduma za kifedha katika mnyororo wa thamani na masoko.

Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya TAMFI, Bw Joel Mwakitalu, alisema kwamba “tuzo hizi ni chachu kwa
wajasiriamali na wanachi kwa ujumla na kwamba kukopa na kurejesha katika
biashara ni ufunguo wa maendeleo ya ki-uchumi.”

Aliongeza kwamba
“kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya wajasiriamali 30 wamenufaika na tuzo
hizi. Wajasiriamali hawa walipita katika mchujo uliokuwa na vigezo vya
urejeshaji wa mikopo kwa muda uliopangwa, ukuaji wa biashara, ubunifu katika
biashara, uzalishaji wa ajira, na bishara endelvu.

Miongoni mwa
wajasirimali waliofaidika na fedha hizo walikuwepo katika hafla ya uzinduzi kwa
msimu wa 2018/19.

Wajasiriamali hawa
waliopita kwenye mashindano haya walipata Zaidi ya Shillingi Milioni 140 ambazo
tafiti zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya pesa hizi za tuzo zimeziwekeza kwenye
biashara zao.”
 

Tuzo hizi
zitazingatia maeneo ya kijiografia, jinsia, na sekta za uchumi. Biashara
itakayoshindanishwa ni lazima iwe endelevu, inaleta mabadiliko katika maisha ya
mjasiriamali na jamii inayomzunguka. Kutakuwa na mshindi wa jumla na mshindi
kutoka taasisi inayotoa huduma ndogo za fedha.

VIGEZO VYA TUZO

Wajasirimali
wadogo wenye mafanikio ni lazima wawe wale ambao kwa juhudi binafsi
wamesababisha mabadiliko makubwa katika shughuli zao, katika jamii na familia
zao.

 

Maombi ya ushiriki
yatachambuliwa kwa kuangalia yafuatayo:

Ukuaji wa kibiashara: Mjasirimali anatakiwa kuelezea historia ya
biashara, ikoje kwa sasa, ilianza linin a ilianzishwaje, mapato na ukubwa wa
mauzo wakati ananza na sasa na kiasi kinachouzwa kwa mwezi. Kwa sasa kuna
matawi mangapi ukilinganisha na wakati alipoanza au kama utoaji huduma huo
umetanuliwa au kubadilishwa.

 Kutambua msukumo
ulioletwa na biashara hiyo kwa biashara nyingine na faida ambazo wanunuzi au
wateja wamezipata kutokana na kukua kwa biashara na kama biashara hizo zipi
ndani ya jamii, nje ya wilaya au mbali zaidi.

 Uzalishaji wa ajira: je biashara imepanda kutoka kuwa na ajira
ya mtu mmoja na kuajiri watuw engi wakiwemo wale ambao si wa familia moja.

Watu wangapi
waliajiriwa wakati wa kuanza na sasa wapo wangapi. Je jinsia katika ajira
zikoje.

 Uendelevu: je uendeshaji wa biashgara hiyo unaenda
sawa na  gharama zake, je imesajiliwa au
inafikiriwa kusajiriwa?

Je inategemea
mafanikio ya mjasirimali au inajitegenmea na endelevu kwa kuzingatia msiungi
uliowekwa?

 Ubunifu: je ni kitu gani kinafanywa tofauti ili kuifanya biashara kuwa
na mafanikio?Je inatoa bidhaa adhimu? Je wameanzisha mawasilino ya Tehama au
uhifadhi wa nishati ili kuendelezwa kwa ufanisi?

Nidhamu ya kifedha: je mshiriki ameonesha nidhamu ya fedha na
hasa katika uwekaji wa akiba, urejeshaji wa mikopo na uwekezaji. Hapa anatakiw
akuleta taarifa kamili inayohusu mikopo na akiba na historia yake.

Manufaa kwa familia: Ni kwa namna gani biashara hiyo imeleta
athari chanya kwa jamii.  Je mafanikio ya
biashara hiyo imewezesha kuboresha makazi, huduma za afya, elimu kwa watoto,
afya  na kadhalika. Onesha na mifano.

 

Share.

About Author

Leave A Reply