Tuesday, August 20

CCM IRINGA : MBUNGE MSIGWA NI DHAIFU HAWEZI KUSHINDA TENA KUWA MBUNGE

0


 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa
Ramadhani Baraza
akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Iringa

 

 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  

CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa
wa Iringa kimewataka wanachama na wadau wa chama hicho kuupuza ujumbe wa mbunge
wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa kuwa chama hicho kipo imara na sio dhaifu.

 

 

Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa
Ramadhani Baraza
alisema kuwa mbunge huyo anatakiwa kufanya
mkutano wa hadhara kuwaaga wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kuwa zama za
kuiongoza manispaa ya Iringa umefika kikomo.

 

 

“Zama za Msigwa zimeisha
kuongoza manispaa ya Iringa kwa kuwa wananchi wameshamchoka kwa kuwa sio
kiongozi aliyewasaidia kuleta maendeleo kwani toka aingie madarakani hajawahi
kufanya maendeleo yeyeto yale kwenye jimbo hili la Iringa” alisema
Baraza

 

 

Baraza alisema kuwa chama cha
mapinduzi kinasema hivyo kwa kuwa chama cha mapinduzi kipo imara kweli kutokana
na aina ya uongozi walionao na mfumo wa siasa ambao wamekuwa wakiutumia
kuwafikia wananchi wa mkoa wa Iringa.

 

 

“Saizi tumefanikiwa kuwafikia
wananchi wa chini kabisa ambao kunakipindi huwa wanasaulika wakati ndio wapiga
kura wetu hivyo tumerudi tumejipanga na tunaendelea kufikia kila siku kwa
kupokea changamoto zao” alisema
Baraza

 

 

Lakini pia Baraza alisema kuwa
wapinzani wamekuwa hawana jambo jipya ambalo wanaweza kuliteleza kwa kuwa
serikali ya chama cha mapinduzi kimesimamia vilivyo serikali na kuhakikisha
wanatatua changamoto za wananchi waliowapa mamlaka ya kuwaongoza.

 

 

“Wapinzani saizi kazi yao ni
kueneza propaganda chafu ambazo sasa wananchi wamezichoka na hazina nafasi
kwenye ulingo wa siasa safi na yakuleta maendeleo kwa wananchi” alisema
Baraza

 

 

Baraza alisema kuwa chama cha mapinduzi sio
dhaifu kwa kuwa kimefanikiwa kupata madiwani saba ambao wameamia kwenye chama
cha mapinduzi kwa ajili ya udhaifu wa CHADEMA
na viongozi wake wa mkoa wa Iringa.

 

 

“Moto wetu ndio kwanza umeanza hivyo tumwambie Msigwa
ajipange kuondoka kwa kuwa saizi ameshakuwa dhaifu na hana jambo jipya ambalo
linaweza kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa” alisema Baraza

 

 

Hoja hiyo imekuja siku kadhaa  baada mbunge wa jimbo la Iringa kusema kuwa
chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa ni dhaifu na hakiwezi kumuondoa madarakani
labda yeye aamue kung’atuka kwa hiyari yake.

Share.

About Author

Leave A Reply