Friday, July 19

AZILONGWA AWAFUNDA VIJANA CHIPUKIZI KUSOMA KWA BIDII

0


IMG-20181113-WA0010

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

 

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kibaha Mjini mkoani Pwani ,umetoa rai kwa watoto na vijana chipukizi kujiendelea kitaaluma licha ya kujiingiza kwenye siasa ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani .

 

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Umoja huo ,Azilongwa Bohari wakati wa uchaguzi wa chipukizi kwenye wilaya hiyo .

Alisema,vijana wanapaswa kuandaliwa kisiasa kwani bila ya kuwaandaa kiuongozi kunasababisha kuwa na viongozi wasio na maadili na wasio na utawala bora na wazalendo.

Aidha Azilongwa, alitoa madaftari na mafaili kwa chipukizi hao ili kuwapa molari ya kuendelea kupenda masomo kwani siasa bila kisomo haiwezekani.

“Hata Rais dkt.John Magufuli ndio maana alitoa agizo la elimu bure mashuleni kuanzia msingi hadi kidato cha nne ili kupunguza wimbi la watoto wa mitaani “

 

“Hili ni agizo kutoka taifa maana tunawaandaa vijana ambao baadae watakuwa wazalendo na ari ya kusimamia chama na taifa kijumla”

“Chama Cha Mapinduzi ni chama bora tangu uhuru hivyo tunatarajia nyie kuwa viongozi wenye weledi ,wasomi hatutegemei nyie kuwa mafisadi, wezi na wala rushwa msikubali ,mpambane kwa ajili ya maslahi ya umma na Taifa,” alisema Azilongwa .

 

Azilongwa aliagiza viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo kata kuhakikisha wanawashirikisha chipukizi kwenye vikao ambavyo wanapaswa kushiriki pasipo kuwasahau kwakuwa wanachangamoto ambazo wataziwasilisha kwenye vikao hivyo.

Nae katibu mwenezi wa CCM Kibaha Mjini, Elias Masenga alieleza, vijana wana nafasi kubwa ya kuwa viongozi kwani hata Rais ameonyesha imani kubwa kwao kwa kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali.

 

Awali katibu wa umoja wa Vijana UCCM Kibaha Mjini Amina Makona, alisema Chipukizi ni wanafunzi wanapaswa kusoma,kuwa watiifu ,kusaidia wazazi na kujiepusha kujiingiza katika makundi yasiyo na maadili na magenge ya kuvuta madawa ya kulevya. 

 

Kwenye uchaguzi huo nafasi ya mwenyekiti ilichukuliwa na Ismail Bwando .Nafasi ya Wajumbe sita wa chipukizi kuwakilisha ngazi ya mkoa ni Mwanakombo Jumanne , Ally Omary , Asha Mwinshehe ,Seif Moses na Mwinshehe .

Share.

About Author

Leave A Reply