Sunday, August 25

The Bad Boys: Wachezaji 11 waliowahi kuhukumiwa kwenda Jela kwa makosa ya kubaka, madawa, vurugu…

0


Wanasoka wamezoeleka kuwepo kwenye line up za makocha wao, lakini baadhi wamezoeleka kuwepo kwenye line up za polisi pia!.

Hapa, tuangalie wachezaji 11 ambao wamekumbwa na matatizo makubwa ya kisheria – wachezaji wanaunda kikosi hatari lakini kikosi cha wachezaji historia ya makosa ya jinai.

Goalkeeper: Bruno Fernandes

Alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 22 kwa kutoa amri ya mauaji ya mama wa mtoto wake wa kiume.

Bruno alikuwa golikipa tegemeo katika kikosi cha ushindi wa ligi ya Brazil na kikosi cha Flamengo mwaka 2009, na alikuwa akitegemewa huenda akasimama langoni wakati wa kombe la dunia 2014, lakini maamuzi yake ya kimaisha yakaingilia vibaya career yake.

Mwaka 2010 alikutwa na tuhuma za kutoa amri ya kuuwawa kwa Eliza Samudio, mama wa mtoto wake wa kiume Bruninho. Alikutwa na hatia miaka 3 baadae na kuhukumiwa kwenda jela miaka 22. Kilichopelekea Bruno kufanya yote hayo ni kutokuwa na maelewano na Eliza, kitendo kilichopelekea marafiki zake kumteka mwanamke huyo na baadae wakamkata kata vipande vipande na kisha wakawapa vipande hivyo vya mwili mbwa.

Miaka 7 baadae akiwa anatumikia adhabu yake – akashinda rufaa ya kesi na kuachiwa huru na sasa anaitumikia klabu ya Boa Esporte ya daraja la pili – Brazil.

Beki wa kulia: Serge Aurier

Wakati akiwa bado anaitumikia Paris Saint Germain – beki wa Ivory Coast Serge Aurier aliingia kwenye mikono ya sheria baada ya kukutwa na hatua ya kuwashambulia kimwili maofisa ya polisi jijini Paris Ufaransa!

Aurier alihukumiwa kwenda jela kwa miezi 2 na kulipa faini ya millioni 60 za kitanzanja.

Beki wa kati: Ruben Semedo

Beki wa kati wa Villarreal kwa sasa yupo nyuma ya nondo, baada ya kunyimwa dhamana kutokana na kesi yake ya mauaji.

Semedo mwenye umri wa miaka 23, pia ana kesi nyingine za kuiba, kuteka na kushambulia mwili.

Semedo pia alikutwa na silaha ya moto isiyo halali nyumbani kwake baada ya upekuzi wa polisi.

Mcolombia huyu pia ana kesi nyingine ambayo haijaanza ya kufanya vurugu katika klabu ya usiku.

Beki wa kati: Breno Rodrigues

Breno Vinicius Rodrigues – mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Bayern Munich alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 3 na miezi 9 baada ya kukutwa na hatia ya kuchoma moto nyumba aliyokuwa akiishi nchini Ujerumani.

Nyumba hiyo ambayo alikuwa amepangiwa na klabu ya Bayern Munich – iliharibika yote!

Baada ya hukumu kutoka Breno aliwaomba msamaha waajiri waje Bayern na mwenye nyumba kwa kitendo chake – akisema alifikia hatua hiyo kutokana na stress za majeraha yaliyokuwa yakimuandama na kushindwa kuitumikia timu yake.

Beki wa kushoto: Alexis Zarate

Muargentina huyu alikutwa na hatia ya kesi ya ubakaji na kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka 6 na miezi 6.

Zarate alikutwa na hatia ya kumbaka Guiliana Peralta – mpenzi wa mchezaji mwenzie wa klabu ya Independiete Martin Benitez.

Tukio hilo lilitokea mwaka 2014 katika Apartment ya Zarate wakati alipowaalika Guiliana na Martin – ilipofika usiku wakati wamelala – Zarate akamrukia shemeji yake na kumbaka.

Midfielder: Adam Johnson

Moja ya viungo mafundi wa kiingereza alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 6 kwa kosa la kufanya mapenzi na msichana ambaye alikuwa chini umri.

Johnson aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Sunderland alihukumiwa kwenda jela mwaka 2017, tukio hilo la kufanya mapenzi na binti huyo mwenye umri wa miaka 15 lilitokea mwaka 2015 kwenye gari aina ya Range Rover lilokuwa likimilikiwa na Johnson.

Midfielder: Joey Barton

Muingereza mwingine kwenye listi hii ni kiungo Joey Barton ambaye alihukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kesi ya kumshambulia mtu kimwili.

Akiwa na miaka 25 mwaka 2008, Joey Barton alihukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kosa la kufanya mashambulizi – alikutwa na hatia ya kumshambulia mtoto mwenye umri wa miaka 15 kwa kumpiga ngumi ya uso na kumtoa meno, na kesi nyingine alimpiga mtu wakati akitoka klabu ambapo alikuwa kalewa mno a kwenye tukio hili aliungana na ndugu yake Nadine Wilson.

Hata hivyo Burton alikaa jela kwa siku 74 tu na kutolewa kisha akaenda kufanya kazi za jamii.

Wakati huu Barton alikuwa mwajiriwa wa klabu ya Newcastle United.

Midfielder: Yordan Letchkov

Mbulgaria huyu alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 3 kwa kutumia vibaya madaraka yake wakati akiwa meya katika mji wake wa Sliven.

Letchkov ambaye atakumbukwa kwa kufunga goli la ushindi maarufu wa Bulgaria dhidi ya Ujerumani katika mashindano ya kombe la dunia 1994, alikutwa na hatia ya utendaji mbovu wa kazi uliopelekea hasara kubwa katika manispaa ya mji wa Sliven.

Letchkov akiwa na umri wa miaka 44 alihukumiwa jela na kisha akaondolewa kwenye nafasi yake ya umeya.

Midfielder: Ricardo Centurion

Mshambuliaji wa klabu ya Racing Club amekuwa na matatizo ya kisheria kila mara – huko nyuma alishawahi kuwa na tuhuma za kumpiga sana mpenzi wake, lakini sasa ana kesi ya kujibu ya rushwa – hivi karibuni akiwa anaendesha gari huko Lanus Argentina – Ricardo alipita kwenye taa nyekundu kwa kasi na kuhatarisha maisha ya wavuka kwa miguu, alipokamatwa na polisi akagoma kufanyiwa vipimo vya ulevi na kisha akaonekana kwenye camera akitaka kumhonga Polisi ili aachiwe.

Kesi hii inaendelea na inaonekana Ricardo anaelekea nyuma ya nondo kwa muda wa kuanzia mwaka mpaka miaka 6.

Mshambuliaji: Michele Padovano

Mshambuliaji huyu wa kiitaliano alikutwa na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya kutoka Spain kwenda Italy.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus na Crystal Palace, akiwa na rafiki yake Lucas Mosole walikamatwa mnamo 2006 baada ya uchunguzi wa polisi kwa kesi ya kusafirisha madawa ya kulevya kupitia kwenye machungwa yaliyokuwa yakitoka Spain kwenda Turin.

Padovano – akiwa na miaka 45 alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 8 na miezi 8.

Mshambuliaji : Robinho

Mbrazil mwingine kwenye listi yetu ni Robinho – alihukumiwa kwenda jela miaka 9 kwa kosa la kuhusika kwa ubakaji wa kundi dhidi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 22 – tukio lilotokea jijini Milan mwaka 2013.

Hukumu hiyo ya Robinho ilitolewa mwaka jana wakati Robinho akiwa hayupo nchini Italy, alikuwa kwao Brazil akiwa anaitumikia klabu ya Atletico Mineiro na kutokana na sheria za Brazil, hairuhusiwi kwa raia wa nchi hiyo kupelekwa nchini nyingine kufungwa.

Hata hivyo Robinho amekata rufaa dhidi ya kesi hiyo na mpaka sasa rufaa yake inaendelea kusikilizwa wakati yeye yupo nchini Uturuki akicheza katika klabu ya Sivaspor.

Kocha: Elkin Moncada

Kocha huyu ndio alikuwa mwalimu wa kwanza wa soka wa James Rodriguez – alifungwa jela kwa kosa la kufanya mapenzi na watoto.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.