Sunday, August 18

Siku 8️⃣3️⃣ Kabla ya World Cup: Kwanini Brazil ndio timu yenye mafanikio zaidi

0


Tumebakiza takribani miezi miwili na siku 23 kabla ya michuano ya kombe la dunia kunza – mnamo 14 June. Mashindano ya 21 ya dunia yatafunguliwa siku hiyo katika dimba la Luzhniki wakati wenyeji Russia watakapoumana na Russia. Kuanzia leo tutaanza kufanya countdown ya kuelekea Kombe la dunia kwa kuangalia takwimu na rekodi mbalimbali zilizojitokeza katika historia ya mashindano haya.Siku 8️⃣3️⃣ kabla ya World Cup – Mafanikio ya Brazil 🇧🇷 Kama ingekuwa zinatolewa points kila mchezo wa kombe la dunia ambao wamecheza, basi Brazil wangekuwa wamechukua asilimia 8️⃣3️⃣ ya points walizoshindania. Washindi wa mashindano mara 5 – mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002 wameshiriki katika michuano yote 21 ya Kombe la Dunia – Brazil wameshinda mechi nyingi kuliko nchi nyingine yoyote katika mashindano haya: Mechi 70 katika mechi 104, wamefunga magoli 221 katika mechi hizo. Usichokijua mechi ya kwanza ya Brazil katika kombe la dunia iliisha kwa kipigo cha 4-0 dhidi ya Yugoslavia katika mashindano yaliyofanyika nchini Uruguay mwaka 1930. Ushindi wao wa kwanza ulikuja katika mchezo uliofuatia – wakaifunga 4-0 Bolivia. Ushindi wao wa mwisho katika Kombe la dunia ulikuwa katika robo fainali dhidi ya Colombia katika ardhi ya nyumbani 2014. Ushindi mkubwa zaidi wa Brazil katika Kombe la Dunia mpaka kufikia leo ulikuwa wa 7-1 dhidi ya Sweden 🇸🇪 mchezo uliofanyika mwaka 1950 nchini Brazil, wakati mchezo uliokuwa na magoli mengi uliowahusisha Brazil – ulikuwa ushindi wao wa 6-5 dhidi ya Poland – mchezo uliofanyika katika mashindano ya 1938 nchini Ufaransa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.