Sunday, August 18

Barca wataweza kumaliza msimu na La Liga, Pichichi, na Zamora?? Oblak na Ronaldo kikwazo

0


Wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 11 mbele ya Atletico Madrid, sasa inaonekana Barcelona huenda wakashinda taji la La Liga mapema mwezi April, lakini pia wanawinda rekodi ya kuchukua kombe na tuzo nyingine binafsi mbili – PICHICHI kwa mfungaji bora na Zamora kwa golikipa bora.

Tuzo ya Zamora ni tuzo ambayo hushinda golikipa bora wa ligi ambaye anakuwa amefungwa magoli machache katika msimu husika wa La Liga.

Ni timu 5 tu katika historia ya La Liga ambazo ziliweza kushinda La Liga, PICHICHI na Zamora huku wakifunga magoli mengi zaidi na kuruhusu wavu wak kuguswa mara chache – timu hizo ni Athletic Club msimu wa 1929/30, 1943/44 Valencia, vikosi vya Real Madrid vya msimu wa 1960/61, 1962/63 na 1987/88.

Kurudi kwenye form kwa Cristiano Ronaldo kumeanza kurudisha ushindani wa tuzo ya Pichichi kati ya Ronaldo na Messi – lakini La Pulga bado ana faida ya magoli 3 dhidi ya mpinzani wake, Messi akiwa na magoli 25 na Ronaldo 22.

Kwa upande tuzo ya Zamora – Jan Oblak ameshinda tuzo hii kwa misimu miwili iliyopita, lakini Marc-Andre ter Stegen is msimu huu yupo mbele yake akiwa ameruhusu magoli 13 katika mechi 29, wakati Oblak ameruhusu magoli 14 katika mechi 29.

Kwa maana hiyo Barcelona wameruhusu magoli machache kuliko timu yoyote katika LaLiga, pia wamefunga magoli mengi kuliko timu yoyote – magoli 74 wakati Real Madrid wakifunga 73.

Ligi bado imebakiza mechi 9 kumalizika – Barcelona wana nafasi ya kumaliza kwa msimu wa La Liga wakishinda ligi, Tuzo za Zamora na PICHICHI.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.