Saturday, July 20

ZIARA YA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYA YA MKURANGA YAJA NA FURSA YA MKOPO BILA RIBA

0


Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWENYEKITI wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega ameendelea na ziara yake iliyolenga kuhamasisha kuwainua wanawake kiuchumi kupitia jukwaa hilo.

Akizungumza na wanawake akiwa ziarani katika kijiji cha Mwandege bi. Mariamu amesema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo kuwafahamisha wanawake kuhusiana majukumu yanayofanywa na jukwaa hilo tangu kuanzishwa kwake.

Amesema kuwa akiwa kama mweyekiti wa Wilaya hiyo atahakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia ili waweze kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali.Kuhusiana na mikopo kwa wanawake bi. Mariamu amesema kuwa wanachotakiwa kufanya ni kuendeleza miradi yao ili waweze kupata mikopo katika halmashauri zao bila riba.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kowero amesema kuwa amekuwa akifarijika na juhudi za akina mama hao na kuhusu ahadi ya eneo alilohaidi kwa ajili ya biashara lipo tayari na ramani imeandaliwa ambapo soko kubwa litajengwa kwa ajili ya wanawake na vijana.

Ameeleza kuwa frame zaidi ya 1000 zitajengwa na kuchukuliwa na vikundi au mtu mmoja mmoja kwa gharama nafuu kabisa.Aidha amesema kuwa amefanya mazungumzo na benki ya Amana kuhusiana na mikopo ambayo inatoa mikopo bila riba hivyo fursa hiyo wanawake wa Mwandege wasipoteze fursa hiyo ambayo itawasaidia kujikwamua na kuendeleza miradi yao.

Pia amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega kwa juhudi za kimaendeleo anazozileta katika jimbo hilo na ameomba apate maafisa maendeleo 2 pindi soko litakapokamilika.Katika ziara hiyo mwenyekiti wa jukwaa hilo amechangia kiasi cha zaidi ya shilingi laki nne na doti 20 za kanga kwa vikundi vya kijiji cha Mwandege na amewataka akina mama hao kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli na Mbunge wa jimbo hilo katika kujenga maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Mwandege ,ambapo amewaomba kufanya kazi kwa waminifu ili waweze kunufaika na kazi zao na kuongeza pato la Taifa.
Diwani wa kata ya Mwandege wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Adolf Kowero akizungumza na wajasiriamali wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwakabidhi viongozi wa kata ya Mwandege laki nne na doti 20 za kanga kwajili ya mtaji wa vikundi mbalimbali vya kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwaunga mkono wajasiriamali wa kata ya Mwandege.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
Sehemu ya wajasiriamali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika kata ya Mwandege wilayani Mkuranga Mkoani wa Pwani.

Share.

About Author

Leave A Reply