Monday, July 15

WODI YA UZAZI KATIKA KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UFINYU WA JENGO,VITANDA NA WATUMISHI WA AFYA

0


NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

WODI ya uzazi katika kituo cha afya Chalinze,mkoani Pwani inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwepo ufinyu wa jengo hali inayosababisha wakati mwingine akinamama wazazi kusongamana na kulazimika kulala wawili katika kitanda kimoja.

Aidha kina tatizo jingine la upungufu wa vitanda na watumishi wa afya hasa madaktari . Akikabidhiwa msaada wa vifaa vya akinamama waliojifungua kutoka kwa kikundi cha Pwani generation queens ,mganga mfawidhi wa kituo hicho Salama Masukuzi alisema kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa kunatokana na upungufu wa majengo ya wodi ya uzazi pamoja na vitanda .

Alieleza ,kwasasa wapo maafisa tabibu wanne ,madaktari wasaidizi wawili na daktari mmoja ambao bado ni wachache kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora ya kiafya . “Kituo hiki kinapokea wagonjwa mbalimbali na wengine wakitokea kwenye zahanati 44 zinazozunguka halmashauri ya Chalinze suala ambalo linawawia vigumu kutekeleza wajibu wao ” alifafanua Salama .

Alieleza wamepata manesi wanne kupitia ajira mpya, ameishukuru serikali lakini aliiomba kuwaboreshea zaidi huduma ya afya ili kuwahudumia wananchi. Kwa upande wa akinamama wa Chalinze,akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja walisema wanapata shida katika kununua drip,vifaa vya uzazi na kipimo cha kujua wingi wa damu ambacho hutakiwa kwenda nje wakati mjamzito akiwa tayari yupo wodini.

“Tumekuwa tukipata shida ya ukosefu wa vifaa kwa ajili ya kujifungulia na wakati mwingine inatubidi kwenda dukani kununua na uwezo wetu kifedha ni mdogo ,tunqshindwa kumudu gharama za matibabu” Demertia aliwashukuru Pwani generation queens kwa misaada waliyoipata na kuomba wadau na vikundi vingine vikumbuke kusaidia kituo cha afya Chalinze.

Akikabidhi msaada wa vifaa mbali mbali katika wodi ya uzazi kwenye kituo hicho cha afya , Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Queens Betty Msimbe alisema wamesaidia kutokana na kubaini kuwepo kwa upungufu wa vifaa hasa kwa wanawake wajawazito ambao wanakwenda kupatiwa matibabu na kujifungua.

Betty alieleza,wapo wanawake ambao wamekuwa wakipata shida pindi wanapokwenda katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kujifungua hivyo wakaona kuna umuhimu wa kutoa msaada huo

Share.

About Author

Leave A Reply