Saturday, July 20

SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA USIKIVU WA TBC NCHI NZIMA:DKT.MWAKYEMBE

0


Na Shamimu Nyaki –WHUSM.


Katika kuimarisha usikivu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Serikali imeendela kuweka mikakati
mizuri ya kuongeza usikivu wa shirika hilo hapa nchini kutegemea na
upatikanaji wa fedha.


Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini
Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison
Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Zaynab Matitu Vulli
(Viti Maalum) aliyeuliza Ni chanagamoto zipi zinazopelekea TBC
kutosikika katika baadhi ya maeneo ya Pwani ambapo Mhe. Waziri alieleza
kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 maeneo mengi ya nchi yaliongezewa
usikivu.


“TBC ina mitambo ya kurushia
matangazo  ya redio ya masafa ya FM katika Wilaya ya Kisarawe ambayo
hufikisha matangazo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
katika masafa ya  87.8 MHz kwa idhaa ya TBC Taifa, 90.0 MHzkwa idhaa ya
TBC FM na 95.3 kwa idhaa ya TBC International”.Alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha ameongeza kuwa katika Bajeti
ya mwaka 2016/17 TBC ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika
Wilaya tano zilizopo mpakani ambazo ni Wilaya za Longido,
Rombo,Tarime,Nyasa na Kibondo.


Vilevile katika Bajeti ya mwaka
2017/18 mradi wa usikivu katika mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto
mkoani Tanga ulitekelezwa ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu TBC
ilikua na vituo thelathini na tatu vya kurushia matangazo katika masafa
ya FM kwenye Wilaya 102 kati ya 161 nchi nzima.


Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa
Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa TBC inapanua usikivu ambapo kwa
mwaka huu wa fedha maeneo ya Unguja na Pemba,Simiyu,Njombe,Songwe,Lindi
maeneo ya Nangurukuru  pamoja na Mkoa wa Morogoro maeneo ya Morogoro
Vijijini,Bondwa na Mahenge yatafikiwa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa bungeni Jijini Dodoma.

Share.

About Author

Leave A Reply