Saturday, July 20

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA TIMU YA WATAALAMU WA MATIBABU YA MOYO IKULU JIJINI DAR

0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam.  

Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo
cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini
Marekani  Profesa Roger Hartl akizungumza katika kikao kilichowajumuisha
Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka
nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu
jijini Dar es Salaam.  

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
zawadi ya Kitabu alichopewa Dkt. Akiva Tamir Mwakilishi  wa Madaktari
hao kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart kutoka Israel kama Heshma
Maalumu ambayo Taasisi hiyo huitoa kwa watu Maalum.


Madaktari
hao kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart ya Israel pamoja na
Madaktari kutoka Marekani wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya
kuanza mazungumzo yao na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa
zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Profesa Mohamed Janabi mara baada ya mazungumzo ujumbe wa Madakatari
kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart ya Israel pamoja na Madaktari
kutoka Marekani Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa
Barua ya Shukrani Balozi wa Israel hapa nchini Noah Gal Gendler ili
aiwasilishe kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa ajili ya
kushukuru kutokana na mchango wa Taasisi hio ya Save a Child’s Heart.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzungumza nao na kuwashukuru kwa huduma wanayoitoa nchini. Wengine katika picha ni Balozi wa Israel hapa nchini Noah Gal Gendler wanane kutoka (kushoto) waliosimama mstari wa mbele Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Dkt. Faustine Ndungulile watisa kutoka kulia mstari wa mbele.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani  Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani  Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Share.

About Author

Leave A Reply