Saturday, July 20

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

0


 Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungungumza na Watumishi wa Wilaya ya Rombo mara baada ya kupokea
taarifa ya Wilaya hiyo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na
kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)

24

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya
mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo kutoka kwa
Mhandisi wa Halmashauri Mhandisi Boniface Vedasto. Makamu wa Rais yupo
kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani
Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

56

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa
Tarakea waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa njiani kuelekea kwenye
shamba la miti Rongai. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na
kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)

810

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua kitalu cha miche
wakati alipotembelea shamba la miti la Serikali lililopo Rongai Rombo.
Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za
maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

14

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa
Serikali Wilayani Rombo kufanya kazi kwa kushirikiana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Agnes Hokororo.

“Wote tunajenga nyumba inayoitwa
Tanzania katika nafasi yako yoyote ulipo unajenga nyumba inayitwa
Tanzania, kwa itikadi yako yoyote uliyonayo unajenga nyumba inayoitwa
Tanzania tunatawaliwa na sheria moja, tunataliwa na miongozo hiyo hiyo
ya Serikali, kanuni na mambo mengine na hiyo hiyo Serikali”.

Katika ziara yake Wilayani Rombo
Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala
la Halmashauri ya Rombo, mradi wa maji Shimbi Mashariki,kukagua shamba
la Miti Rongai.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye
ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo pia alipata
nafasi ya kuwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza barabarani
kumsalimia na alihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya
msingi Keni-Mengeni.

Kwa upande mwingine Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali hii
inafanya jambo la kihistoria kwa kukamilisha ujenzi wa vituo vya Afya
350.

Share.

About Author

Leave A Reply