Tuesday, July 23

MADIWANI URAMBO WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI TATIZO LA MBOLEA YA TUMBAKU KUCHELEWA

0


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Magreth Nakainga akitioa ufafanuzi kwa Madiwani wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa utekelezaji kwa kila Kata wilayani humo jana.

4a

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo jana.

A

Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta  akichangia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo jana.

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA.

UZALISHAJI na ubora wa tumbaku msimu ujao wa kilimo unaweza kushuka baada ya mbolea ya kukuzia zao hilo kuchewewa kuwafikia wakulima hadi hivi sasa.Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi kwa niaba ya Madiwani wenzake wakati wa kikao cha Baraza hilo.

Alisema hadi hivi sasa mbolea ya aina ya N.P.K bado hajifika kwa wakulima wakati msimu wa mvua umeshakaribia kuanza jambo linalotishia ubora na uzalishaji.Malunkwi alisema kitendo hicho sio tu kitamwathiri mkulima pekee pia mapato ya Halmashauri ya Urambo yataathirika kwa sababu sehemu kubwa inategemea tumbaku ili kupata mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Alisema kwa mujibu wa taarifa za Mzabuni ambayo amepewa jukumu la kusambaza mbolea kwa wakulima wa tumbaku, meli iliyobeba mbolea hiyo itawasili nchini tarehe 11 mwezi huu na inaweza kuchukua wiki mbili na kendelea kuwafikia wakulima jambo ambalo litafanya mazao ya wakulima yapitwe na wakati.

Malunkwi aliomba Serikali kuibana Kampuni ya Mbolea nchini(TFC) kuhakikisha wanaazima mbolea kutoka Kampuni binafisi ili kuziba pengo hilo na kuokoa mazao ya wakulima na hatimaye mbolea yao itakapowasili wazirudishie mbolea yao.

Naye Diwani wa Kata ya Itundu Ahmed Hamoud alisema tatizo hilo la ucheleweshaji wa mbolea ya tumbaku limeanza kuwa sugu kwani kwa kipindi cha miaka mitatu mfufulizo imekuwa ikichelewa kuwafikia wakulima na kuwafanya kuzalisha chini ya ubora na kiwango.

Alisema hatua hiyo imesababisha kushuka kwa makisio ya wakulima kutokana na kushindwa kufikia malengo waliyokubaliana na Kampuni za ununuzi wa tumbaku.Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa alimtaka Mzabuni anayepewa zabuni ya kuagiza mbolea kwa ajili ya wakulima wa tumbaku kuzingatia kalenda ya zao hilo , kinyume cha hapo ni kumuumiza mkulima na kurudisha nyuma juhudi zake za kujiletea maendeleo.

Alisema kuwa Kitendo cha Mazabuni kuchelewesha mbolea kinakwenda kinyume na juhudi za Serikali za kumshika mkono mkulima mdogo mdogo ili hatimaye siku moja naye apige hatua.

Share.

About Author

Leave A Reply