Monday, March 18

MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUTHAMINI MIRADI INAYOFANYWA NA SERIKALINI

0Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani) katika kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao.
Baadhi ya Maafisa Ununuzi na Ugavi wakisikiliza mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akisikiliza kwa makini michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha mada kwa maafisa hao juu ya uvumbuzi na ufanisi bora katika masuala ya ugavi.

Na. Edward Kondela

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Maafisa Ununuzi na Ugavi nchini kutambua na kuthamini miradi mbalimbali inayofanywa na serikali, kwa kuthaminisha miradi hiyo na thamani halisi ya fedha inayotumika katika miradi.

Prof. Gabriel aliyasema hayo leo (05.12.2018) Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mada kuhusu uvumbuzi na ufanisi bora kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakati wa siku ya ufunguzi wa kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao.

“Katika ujenzi wa miradi mikubwa tunayoishuhudia kwa sasa nchini, fedha zinatumika, lakini jinsi gani sasa vifaa vinanunuliwa, malighafi zinanunuliwa ni jambo kubwa sana, kuna haja ya wahusika katika tasnia hii wawe wabunifu kadri iwezekanavyo na wawe ni watu wa kuleta mabadiliko”. Alisema Prof. Gabriel.

Katibu mkuu huyo aliwataka maafisa hao kuwa wavumbuzi na kufanya kazi kwa ufanisi katika masuala ya ugavi na usambazaji bidhaa ili kuisaidia serikali, kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kujenga miradi mbalimbali ili iwe na tija kwa taifa.

Aidha, Prof. Gabriel aliwataka Maafisa Ununuzi na Ugavi, kubadili mienendo yao ambayo haiwaletei tija katika ufanisi wa kazi, pamoja na kujiongezea thamani katika jamii kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Share.

About Author

Leave A Reply