Thursday, August 22

JIACHIE: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA NENO KWA MAWAZIRI WA AFYA WA AFRIKA MASHARIKI,KATI NA KUSINI

0


Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

SERIKALI ya Tanzania imewahakikishia mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini kuwa itaendelea kuisaidia sekretarieti ya ECSA yenye makao makuu yake jijini Arusha.

Imesema kuwa inatambua majukumu ya Sekretarieti hiyo katika sekta ya afya huku ikiwaomba mawaziri hao na wadau wengine kuboresha mifumo ya afya ili kusaidia kuondoa changamoto zinazojitokeza wakati wa utoaji wa huduma bora za afya.

Akizungumza Dar es Salaam jana jioni wakati anafungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka Afrika Mashariki,Kati na Kusini,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni jukumu la Serikali ya Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji na kusaidia sekretarieti ya ECSA.Waziri Mkuu amesema pia mawaziri hao katika mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam wajadili mambo yote muhimu yanayohusu sekta ya afya na kufafanua wasiache hata jambo moja nyuma na zaidi ni nini kifanyike kuboresha sekta ya afya.

“Niwaombe mawaziri wa afya ambao mmekutana katika mkutano huu ,wekeni mikakati yenye lengo la kuboresha sekta ya afya na kuangalia namna ya kuondoa changamoto ambazo zinakuwa vikwazo katika utoaji wa huduma bora za afya.”Boresheni mifumo ya afya na kubwa zaidi ifikapo mwaka 2030 tuwe tumefikia malengo ya Maendeleo Endelevu(SDG’s) katika eneo la afya.

“Jukumu la Serikali ya Tanzania ni kuendelea kusaidia na kuwa mwenyeji wa sekretarieti ya ECSA-HC,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.Ametumia mkutano huo kuwataka mawaziri hao na wadau wengine wa afya ambao wamedhuria mkutano kuweka mkakati wa namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama TB na magonjwa ya kuambukiza.

Mbali ya kuzungumzia mambo yanayohusu uboreshaji wa huduma za afya,Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba washiriki kabla ya kuondoka watembelee vivutio vya utalii vilivyopo nchini.Kwa upande wa baadhi ya washiriki wa mkutano wameelezea hatua wanazochukua kuboresha sekta ya afya huku wakiisifu Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ambavyo upo imara katika usimamizi mzuri wa mambo mbalimbali.Kauli mbiu ya mkutano huo wa 65 kwa mawaziri hao wa afya unasema Ushiriki wa sekta ya afya katika kupata mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu(SDG’s).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya, uliohudhuliwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.