Wednesday, August 21

JIACHIE: WATU 26 wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa ajali iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani .

0


Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake Kimanzichana – Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi 10 ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Inasemekana majeruhi waliopelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wengine wao wamekatika viongo mbalimbali vya mwili.Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya.Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ,aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini .
Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe.
“Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao.” alieleza Ulega.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.