Tuesday, August 20

JIACHIE: WAKAZI WA MWANZA TAMASHA LA PASAKA LINAKUJA ,KAENI MKAO WA KUMTUKUZA MUNGU KWA NJIA YA UIMBAJI NDANI YA CCM KIRUMBA

0


Kampuni ya Msama Promotiosn Ltd inaandaa tamasha la Pasaka kanda ya ziwa likalofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili,litakalohusisha waimbaji wa nyimbo za injili mbalimbali hapa nchini,na kwamba litakuwa tamasha lile lile ambalo limekuwa likifanyika jijini Dar Es Salaam kwa miaka yote. 
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema Tamasha la Pasaka Mwaka huu litafayika jijini Mwanza na mkoa wa Simiyu mnamo Aprili 1 na April 2 na baadaye kuendelea kwenye mikoa mingine. 
“Tamasha la pasaka safari hii linaanzia mkoani Mwanza na baadae mkoa wa Simiyu,na pia mikoa mingine,tamasha hilo kwa jiji la Mwanza litafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, na baadae mkoani Simiyu katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi’’,alisema Msama. 
Msama amesema kuwa tamasha hilo kwa Mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa,kwa maana ya eneo lakini mambo yote yaliyokuwa yikifanyika jijini Dar,yatahamia jijini Mwanza. 

Msama anawakaribisha wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake,kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia utukufu wa Mungu kwa njia ya kuimba kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili . 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ,Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,alipokuwa akieleza kuhusu mwanzo wa maandalizi ya tamasha la pasaka 2018,litakaloanzia kanda ya ziwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.