Sunday, August 25

JIACHIE: MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA ABDALLA MZEE PEMBA

0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba. Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi. Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.

Kwa Upende wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi kufanya kazi kwa taratibu na sheria lakini pia alitoa wasihi kwa wanasiasa wanaochochea vurugu kwani wao watachukuliwa kama wahalifu na si wanasiasa. Ziara ya Makamu wa Rais imekamilika leo ambapo pia alitembelea Hospitali ya Abdala Mzee ambapo alijionea vifaa vya kisasa vilivyowekwa na huduma bora zinazotolewa.

Makamu wa Rais pia aliweka mawe ya Msingi katika ujenzi wa madarasa katika skuli ya sekondari ya Ali Khamis Camp pamoja na ujenzi wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Ole. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Hafidh Jabir Ali mwenye umri wa miaka 3 aliyelazwa kutokana na kuungua na chai katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Rayna Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja aliyelazwa kutokana na kuungua moto katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Wuxiao Shu juu ya matibabu ya mguu wa mtoto AzarAli mwenye umri wa miaka aliyelazwa  katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi nje ya majengo ya hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya hospitali hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Read More

Share.

About Author

Comments are closed.