Sunday, August 18

JIACHIE: KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE CHAFUNGWA KWA KUKOSA SOKO

0


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

KIWANDA cha kutengeneza nguzo za zege cha Hunnan Power ,mjini Kibaha Mkoani Pwani ,kimefungwa kutokana na kukosa tenda na soko , tangu uzalishaji uanze mwezi september mwaka jana.

Kutokana na hali hiyo, kiwanda hicho kimebaki gofu na kupunguza ajira kutoka wafanyakazi 30 hadi wawili kwasasa.Hayo yalibainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alipotembelea viwanda nane vilivyoanza uzalishaji na ambavyo vipo kwenye hatua za ujenzi mjini Kibaha.
Alisema mkoa huo unadhamira ya kuwa ukanda wa Viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali lakini endapo soko litakuwa hakuna ,wawekezaji watakata tamaa.Alisema mkoa una viwanda vinavyotengeneza nguzo za zege viwili ikiwemo Hunnan Power /Kibaha na East Africa infrastructure engineering Ltd kilichopo Fukayosi /Bagamoyo ambavyo vinahofiwa kushindwa kuendelea kuzalisha kwasababu ya bidhaa zake kukosa wateja.
“Katika ziara hii tumebaini changamoto ya kiwanda cha Hunnan Power kukosa masoko na tenda huko shirika la umeme (Tanesco ),hawajapata tenda mara tatu ,”“Hali hiyo imesababisha kiwanda hicho kufungwa, hakizalishi ,mashine zimefungiwa ndani ,kiwanda kimezungukwa nyasi ,kimekuwa gofu na ajira hakuna” suala hili linaangusha juhudi za rais John Magufuli ,Mkoa na serikali”alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo alieleza, wawekezaji wanajitoa kuunga mkono na kuitikia wito wa serikali kujenga viwanda lakini baadhi vinakumbana na changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika.Aliahidi kuzungumza na waziri mwenye dhamana na mkoa utafuatilia ili waziri wa nishati aweze kusaidia suala hilo.
Mkuu huyo wa mkoa aliitakaTanesco kuangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo na kuangalia namna ya kutoa tenda ili kuokoa kuinua viwanda hivyo.Mhandisi Ndikilo alitaja changamoto nyingine alizofikishiwa kwenye ziara hiyo,kuwa ni umeme,maji barabara na vibali kutoka TFDA.Aliwasihi viongozi wa wilaya ,halmashauri kuandika barua moja kwa moja kwa taasisi husika watatue matatizo hayo ili kuwavutia wawekezaji .“Official communication itasaidia kuliko kusumbua sana hawa wawekezaji ,,itakuwa rahisi kufanya ufuatiliaji na kuzibana taasisi husika na kuzisukuma zifanye utekelezaji ” alisisitiza.
Awali akitoa taarifa ya kiwanda cha Hunnan Power ,mkalimani wa kiwandani hapo, Suleiman Ramadhani alisema kiwanda kilianza ujenzi Jan 2017 na kuanza uzalishaji September 2017 na kimegharimu dollar milioni mbili na hakijawahi kuuza hata nguzo moja.Alisema kiwanda hakifanyi kazi tangu Jan mwaka huu kwakuwa kinategemea tenda na soko .
Suleiman alielezea kuwa ,wenye viwanda wanahitaji kujenga kiwanda kingine katika eneo hilo lakini wanashindwa kwasasa hadi hapo watakapopata wateja .Mhandisi wa udhibiti wa mapato Tanesco mkoani Pwani ,Fabian Rukiko ,alisema hawajawahi kutumia nguzo za zege mkoani hapo hadi hapo itakapohitajika.
Alikishauri kiwanda hicho kujitangaza kupitia kitengo cha mauzo na masoko kwani itasaidia kufanya ufuatiliaji na kushirikiana na wadau wakubwa watakaoweza kununua bidhaa hiyo muhimu ambayo inadumu kwa kipindi kirefu.Mwezi Novemba 2017, waziri wa Nishati Dk.Merdard Kalemani alitembelea kiwanda cha nguzo za zege kilichopo Fukayosi na alilitaka shirika la umeme Tanesco kutumia nguzo zinazozalishwa nchini kwenye ujenzi wa miradi mikubwa.
Nanukuu”:”baada ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa nguzo za umeme toka nchi za nje na kuruhusu wawekezaji kutengeneza nchini, sasa umefika wakati TANESCO ianze kutumia nguzo za zege kuanzia Desemba 2017 kwenye miradi mikubwa”;alisema.
Kiwanda cha Hunnan Power kinachotengeneza nguzo za zege mjini Kibaha, kikionekana kutoweza kuendelea na uzalishaji kutokana na kukosa soko na tenda ,na nguzo zikionekana kubaki chini bila mauzo ,wakati mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,alipofanya ziara yake ya siku moja kutembelea viwanda nane mjini hapo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,alipofanya ziara yake ya siku moja kutembelea viwanda nane mjini Kibaha ambavyo vingine vianza uzalishaji na vingine vikiwa hatua mbalimbali za ujenzi (picha na Mwamvua Mwinyi)Read More

Share.

About Author

Comments are closed.