Monday, July 15

CHIRWA ASAINI RASMI AZAM, AAHIDI KUIFANYIA MAKUBWA AZAM

0


Na Agness Francis, Globu   ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam fc umefanikiwa  kuinasa saini ya mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Ni baada ya dili lake la kurudi Yanga kugonga mwamba.

Uongozi  wa Azam FC umesema kuwa usajili wa Chirwa ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam chini ya kocha mkuu Hans Van der Plujim katika kuboresha eneo la ushambuliaji la  kikosi hicho. 

Chirwa amejiunga na Azam baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo alisajiliwa hivi karibuni.Mshambuliaji huyo ametua Azam akiwa ameshawahi pia kuichezea Yanga na kisha baadaye kukimbilia huko Uarabuni baada ya mambo ya kifedha na mabingwa hao wa kihistoria kutokuwa sawa.

Baada ya kurejea nchini, awali ilielezwa Chirwa angeweza kurudi Yanga lakini mambo yamekwenda tofauti.Kupitia ukurasa wa Istagram wa klabu ya Yanga,  Uongozi huo umebainisha  kuwa awali mshambuliaji  huyo alikuwa arejee klabuni  licha ya kocha mkuu wa  klabu hiyo mwinyi Zakhera kupinga usajiri wake.“Kilichomkwamisha Chirwa kurudi Jangwani ni dau la mshahara alilotaka kulipwa alitaja kiasi kikubwa  cha fedha ambacho Yanga hawakukubali”

Licha ya Octoba 20  mwaka huu Chirwa  alionekana  uwanja wa Taifa katika uchezo uliopigwa na Yanga dhidi ya Alliance  akiwa na kaimu katibu Mkuu wa Yanga Omary  Kaya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Husein Nyika na Mdau mkubwa  Yanga  Abbas Tarimba, ambapo pia aliingia vyumba vya kubadilishia nguo na kusalimiana na wachezaji wa Yanga

Chirwa sasa ataanza rasmi kuitumikia Azam kuanzia Novemba 15 2018 ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa limeshafunguliwa.Na baada ya kutambulishwa, Chirwa amesema kwamba amejiunga na Azam FC kukiongezea nguvu kikosi ambacho tayari ni bora ili wafanikishe azam ya kutwaa mataji.Kwa upande wake, kocha Pluijm ambaye alifanya kazi na Chirwa katika klabu ya Yanga, alisema kwamba  amefurahi sana kumpata mchezaji huyo anayejituma na mwenye bidii kubwa uwanjani.

Chirwa sasa anakwenda kukutana na mshambuliaji raia wa Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyewahi kufanya naye kazi FC Platinums ya Zimbabwe na Yanga.Kama ilivyokuwa Yanga, Ngoma alianza kuja na baadaye akamvuta Chirwa akimshawishi Pluijm aje kuongeza nguvu na kwa Azam hivyo pia, inaaminika Donald amemshawishi tena Pluijm kumsajili mchezaji huyo. .

Mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa akikabidhiwa Jezi ya timu ya Azam fc na Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Hans Van De Plujim mara baada ya kusaini kandarasi za kutumikia  klabu hiyo  kwa mwaka mmoja leo Jijini Dar es Salaam.

Share.

About Author

Leave A Reply