Monday, August 19

ALGERIA KUTUMA MAIMAMU 150 KUONGOZA IBADA NCHI ZA ULAYA MWEZI WA RAMADHANI

0Serikali ya Algeria imesema kuwa itatuma maimamu 150 nchini Ufaransa kwa ajili ya kuongoza ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa hiyo ilitolewa Alhamis na waziri anayehusika na masuala ya kidini Mohamed Aissa.


Waziri huyo amefahamisha kuwa waliochaguliwa ni maimamu ambao wamehifadhi kitabu kitakatifu cha Quran na wenye uwezo wa kufikisha ujumbe katika hutba.

Maimamu hao wanatakiwa kuwa mabalozi wa amani  na uislamu kwa kutoa hutba zisizokuwa na misimamo mikali na isiyoeleweka.

Hayo yalifahamishwa baada ya kiongozi huyo kufanya mazungumzo na  waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerard Collomb na waziri wa mambo ya ndani wa Algeria  Nuredine Bedui.

Maimamu 100 ndio watakaoendesha ibada nchini Ufaransa huku wengine 50 waliobaki kupelekwa nchini Ujerumani, Italia, Uingereza, Ubelgiji na Canada.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.