Thursday, August 22

Tundu Lissu: Narudi Nyumbani Septemba 7

0


Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D, Dodoma.

Lissu ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa gongo moja akizungumza na wapiga kura wake mwishoni mwa wiki kupitia simu ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anarudi nchini Septemba 7, 2019.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Mei 22, 2019 Mnadhimu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema, “Narudi nyumbani Septemba 7 ya anniversary ya kushambuliwa kwangu.”

Share.

About Author

Leave A Reply