Sunday, August 18

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano Felix, Zaha, Sane, Trippier, Gattuso, Mahrez, Hudson-Odoi, Coutinho, Richarlison

0


Kwa upande mwingine , Ronaldo ameidhinisha dau la £100m la mabingwa wa championi Serie A kwa Mreno mwenzake Felix, ambaye ana mkataba wa euro 120m. (A Bola, via Metro)

Crystal Palace watatakiwa kushusha bei yao ya £75m wanayotaka kumtoa Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 26 ikiwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast anataka kuhamia katika klabu ya Championi Ligi. Tottenham, Arsenal na Manchester United wogte wanamtaka lakini wanataka mkataba mzuri. (Star)

Manchester City wanahofu kuwa winga wao Mjerumani Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 23, anaagalia uwezekano wa kuondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kwamba mazungumzo ya mkataba wake yamekwama (Metro)

Manchester United wamemchagua mchezaji wa safu ya kulia nyuma wa timu ya Uingereza ya Tottenham Kieran Trippier, mwenye umri wa miaka 28, kama mchezaji mbadala wanaelenga kumchukua ikiwa watashindwa kusainimkataba na Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21,kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Kwa upande mwingine , United wanaamini Mbeljgiji Thomas Meunier mwenye umri wa miaka 27 anayechezea Paris St-Germain safu ya nyuma kulia ni mchezaji ambaye anayeweza kupatikana kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi anayeweza kukaba nafasi ya Trippier au Wan-Bissaka. (Independent)

Liverpool watadai 40m euros kwa Mserbia Marko Grujic mwenye umri wa miaka 23 -kiungo wa kati huku klabu ya Uhispani ya Atletico Madrid ikionyesha nia ya kumtaka. (ESPN)

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa AC Milan Mtaliano Gennaro Gattuso, mwenye umri wa miaka 41, kuchukua nafasi ya kocha wao Muhispania Rafael Benitez ambaye zaza ana umri wa miaka 59 ikiwa ataamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Gazzetta – in Italian)

Mshambuliaji wa Manchester City Riyad Mahrez anatishia kuondoka kwenye klabu hiyo na winga huyo Mualgeria mwqenye umri wa miaka 28, amekwisha lalamika wazi juu ya kunyimwa muda wa kucheza chini ya meneja Pep Guardiola. (Mail)

Hali ya baadae ya mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, itategemea ikiwa Fifa itaamua kuchelewesha marufuku ya kuhama dhidi ya Chelsea, huku Manchester United pia wakiwafuatilia kwa karibu wachezaji huyo maarufu wa Brazil . (Mirror)

Mlindalango wa Atletico- Madrid Jan Oblak mwenye umri wa miaka 29- raia wa Slovenia ni goli kipa namba moja katika orodha ya Manchester United ya walinda lango wanaoweza kukaba nafasi ya David de Gea wakati hatma ya Muhispania huyo mwenye umri wa miaka 28 katika Old Trafford ikiwa haieleweki. (Metro)

AC Milan wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa Everton Mbrazili Richarlison,mwenye umri wa miaka 21, hata hivyo klabu hiyo ya mabingwa wa Ligi ya Utaliano watatakiwa kuingia Championi Ligi na kulipa 75m euro kwa mujibu wa tathmini ya Ligi ya Primia. (Calciomercato)

Share.

About Author

Leave A Reply