Thursday, August 22

Rayvanny Afunguka Kuhusu Ubabe wa Diamond Ndani ya WCB

0


Msanii Rayvanny kutoka WCB amesema katika utendaji kazi wake na Diamond ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Makulusa’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.

“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema Rayvanny.

Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.