Thursday, August 22

RAY KIGOSI AFUNGUKIA KIPAJI CHA MTOTO WAKE JAYDEN

0


RAY KIGOSI AFUNGUKIA KIPAJI CHA MTOTO WAKE JAYDEN – MWANAHARAKATI MZALENDO ™

New

Staa wa Bongo Movie,  Vincent Kigosi “Ray Kigosi” ametaja siri za mtoto wake kuwa ni mwenye vipaji vya kipekee na nidhamu ya hali ya juu kwa wazazi wake, licha ya umri wake mdogo.Ray amesema pamoja na jukumu la wazazi kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika misingi bora, lakini anajivunia kuona kijana wake akiwa mwelewa wa mambo kwa uharaka zaidi na msikivu.


Ni kweli lazima chako ukisifie lakini ninachokiona kwa mwanangu atakuja kuwa mtoto mwenye kipaji cha kipekee, kwanza katika malezi situmii nguvu kubwa kumwelewesha, amekuwa msikivu na ana nidhamu sana kwa kila mtu,” alisema Ray akinukuliwa na gazeti la Dimba hivi karibuni.


Katika hatua nyingine, Ray ameshindwa kutaja kipaji cha mtoto huyo na kudai endapo atafuata nyayo za wazazi wake kwa kuwa msanii, ni jambo zuri na atahakikisha anakilea kipaji chake ili kumpa mwanzo mzuri wa kufikia malengo yake.

Share.

About Author

Leave A Reply