Sunday, August 25

Rais Magufuli Ameambatana Na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kuelekea Afrika Kusini Kushuhudia Kuapishwa Kwa Ramaphosa

0


Rais John Magufuli leo Ijumaa Mei 24, 2019 ameondoka nchini akiongozana na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuelekea Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa zitakazofanyika kesho.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi pia ameambatana na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

Viongozi hao wametumia ndege ya Shirika la Ndege Tanznaia (ATCL) kwenda Afrika Kusini.

“Baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Afrika Kusini, Rais Magufuli pia anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya kitaifa nchini Namibia ambapo atazindua mtaa uliopewa jina la baba wa Taifa, Julius Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa Taifa hilo,” inaeleza taarifa hiyo.

Share.

About Author

Leave A Reply