Thursday, August 22

Profesa Jay Afunguka Tetesi za Kuachana na Muziki

0


Msanii Joseph haule amefunguka na kusema kuwa kamwe hatoacha muziki kwa sababu muziki ndio uliomfanya kujulikana na mashabiki zake wa miukumi na kumpeleka bungeni, hivyo kuacha muziki ni kama kuwasaliti wananchi wake waliomwamini kupiyia muziki huo..

Joseph Haule kwa jina maarufu Profesa Jay ni wasanii wa kwanza mbao sasa hivi ni wakongwe katika sanaa, lakini pamoja na kwamba aliamua kujiingiza katika siasa, anasema kuwa kazi ya muziki ndio iliyomfanya kujuliakna tanzania na kot ulimwenguni na inawezekana kama sio muziki basi hasingeweza kuwa mbunge wala kujuana na wananchi wa mikumi.

“pagamisa ni kazi nzuri ambayo imepokelwa vizuri tu na mashabiki wangu,miaka yote ya muziki wangu nitaendelea kutoa kazi nzuri za muziki wangu na kamwe siwezi kuacha kazi ya muziki kwa sababu ya kufanya hivyo ni kama kuwasaliti wananchi ambao wamenipeleka mjengoni kupitia muziki huu ambao naufanya.-Alisema Profesa Jay ambae alikuwa studio kutambulishwa wimbo wake mpya”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.