Saturday, August 24

PIERRE LIQUID AKABIDHI MADAWATI 20 KISARAWE

0


Peter Mollel maarufu Pierre Liquid aliyejizolea umaarufu mitandaoni kwa misemo mbalimbali.

Machi 30 wakati wa hafla ya kukusanya fedha kwa ajili ya kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe, Pierre aliahidi kuchangia Sh 100,000 kufanikisha kampeni hiyo inayoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Leo ahadi hiyo imetimia na huenda ikawa ni zaidi ya kile alichokiahidi, Jokate amethibitisha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate ameweka picha inayomuonyesha akipokea madawati 20 kutoka kwa Pierre na kampuni ya fanicha anayofanyia kazi.

Ameandika,” Nimepokea madawati 20 yenye kiwango cha juu kutoka kwa Pierre na kampuni ya Afro Furnishers and Hardware. Kwenye harambee aliahidi kutoa Sh100,000 lakini leo amekuja na madawati.”

Share.

About Author

Leave A Reply