Thursday, August 22

Niva:Irene Uwoya, Wema Sepetu, Shilole na Shamsa Wameaacha Kuigiza

0


Staa wa Bongo Movie, Niva ‘Supermariyoo’  amedai kuwa wasanii wenzake Irene Uwoya, Wema Sepetu, Shilole na Shamsa wameaacha kuigiza na kwasasa wameacha kuigiza sababu wamejikita kwenye mswala mengine.

Akiwataka wanawake wenye vipaji  vya kuigiza wajitokeze kwa wingi  Niva alisema “Irene Uwoya huyu amefungua bar kuigiza kaacha, Shilole kafungua mgahawa nayeye kaacha kuigiza, Shamsa Ford kafungua duka kuigiza kaacha na Wema Sepetu kafungua duka la watoto nayeye hafanyi filamu. Kama kuna mabinti huko mtaani na wanavipaji vya kuigiza basi wafanye mazoezi kwa bidii na waje kujaza nafasi za hawa dada zetu ambao kwa sasa hawaigizi tena” Niva alieleza.

Niva ni moja ya wasanii wakiume wanaotamba kwa sasa kwenye tasnia ya filamu hapa Bongo.

Share.

About Author

Leave A Reply