Monday, June 17

Naondoka Genk, Naenda England- Mbwana Samatta

0


Mchezaji wa timu ya Genk ya ubelgiji  na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameeleza nia yake ya kuondaka kwenye timu yake ya Genk na kuwenda kucheza kwenye ligi ya ueingereza.

Mbali na mashabiki wa Genk kutaka Stamatta abakie kwao kwa ajili ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao baaada ya kufunga mabao zaidi ya 30 katika michuano mbalimbali msimu huu Ulaya. Samatta  amefunguka kuwa anatarajia kuondoka mwishoni mwa msimu huu alipoulizwa  na mwandishi wa gazeti la Mwanaspoti.

“Ndiyo, nitaondoka mwishoni mwa msimu huu,” alijibu Samatta.

Jibu lake linakata kiu ya haraka haraka kwa mashabiki wa soka. “Kuna klabu kama sita za England ambazo zinanifukuzia. Moja inanifukuzia sana na imekuwa ikipiga simu kwa wakala wangu kila siku,” anasema Samatta.

“Kwa sasa sipo katika nafasi nzuri ya kuelezea ni klabu gani lakini pia kuna klabu nyingine mbili kutoka Hispania ambazo zimekuwa zikiisaka saini yangu. Hata hivyo, mimi ndoto zangu ni kucheza katika Ligi Kuu ya England.” anaongeza Samatta.

Samatta anathibitisha kwamba kulikuwa na ofa kutoka katika klabu ya Cardiff katika dirisha la Januari lakini Genk waliitupa kapuni. Vyombo vya habari vya England viliripoti kuwa dau lililotiwa kapuni ni Pauni 13 milioni. Wakala wake mwanamke anayeishi England ndiye ambaye anapokea ofa zote.

Share.

About Author

Leave A Reply