Friday, August 23

MWENENDO WA KESI YA WEMA WEPETU, YAWEZA KUFUTWA

0


Wema ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mitandaoni ya kijamii wa Istagramu kinyume cha sheria.

Uamuzi huo, umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakaka kuwa shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi yupo mkoani Morogoro kikazi.

” Natoa ahirisho la mwisho, upande wa mashtaka, tarehe ijayo kama mtakuwa hamna shahidi muiondoke kesi hii mahakamani hapa au vinginevyo mimi nitaifuta kesi hii” alisema Hakimu Maira.

Hiyo ni mara ya pili kwa kesi hiyo kushindwa kuendelea mahakamani hapo ikiwa katika hatua ya ushahidi, kwani Machi 18, mwaka huu iliahirishwa kutokana na upande wa mashtaka kukosa shahidi.

Awali, wakili wa Serikali, Gloria Mwenda, alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi lakini, Shahidi ambaye walimtegemea kutoa ushahidi yupo mkoani Morogoro kikaza.

Gloria alimtaja shahidi huyo kuwa ni Frank Bizuro ambaye ni Ofisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini ( TCRA).

Hakimu Kasonde baada kupitia maelezo ya upande wa mashtaka, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 14, mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea na kuutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi wa kutosha ili kesi hiyo iweze kuendelea.

Wema, alifikishwa kwa mara ya kwanza Kisutu, Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka hilo.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.

Katika kesi ya msingi, Wema anadaiwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika mtandaoni wake wa kijamii wa Instagram.

Hata hivyo, siku alivyosomewa maelezo ya awali( PH), Wema alikubali kuwa yeye anakaa Mbezi Salasala na anamiliki mtandao wa kijamii wa Istagramu wenye jina la Wemasepetu.

Katika maelezo hayo ya awali, Wema alikana kurekodi video ya ngono ambayo haina maudhui kupitia simu yake ya kiganjani.

Alikiri kukamatwa Oktoba 29, 2018 na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi(Central) kwa ajili ya kuhojiwa.

Pia alikubali kuwa alifikishwa Mahakama ya Kisutu, Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka linalomkabili.

Lakini alikana kusambaza video hiyo katika akaunti yake ya Istagram, wakati akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Share.

About Author

Leave A Reply