Saturday, August 24

Mimi Mars Amtamania Vanessa Mdee

0


Mimi Mars Amtamania Vanessa Mdee – MWANAHARAKATI MZALENDO ™

New

Staa wa Bongofleva, Marianne Mdee, maarufu kama Mimi Mars, amefunguka kuwa moja ya mambo yanayomnyima usingizi ni kutamani kuyafikia mafanikio ya dada yake, Vanessa Mdee.


Mimi Mars, ambaye amekuwa akifananishwa na Vanessa na kudaiwa kubebwa na dada yake, amesema mafanikio ya ndugu yake yanamnyima usingizi kiasi cha kutamani kuyafikia kwa gharama yoyote.
 

“Ukweli ni kwamba Vanessa amekuwa ‘role model’ wangu wa muda mrefu, muziki wake umemkutanisha na wengi na hata mimi kufika hapa ni juhudi zake pamoja na ubunifu wangu, natamani sana siku moja na mimi nikutane na wasanii wakubwa kama ilivyo kwake na pia niweze kutimiza kile ninachokikusudia” alisema Mimi Mars.

Share.

About Author

Leave A Reply