Thursday, August 22

Mama Mobeto Afungukia Sakata la Hamisa Kushindwa Kulipa Kodi na Kuhama Mjengoni

0


Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii picha za nyumba hiyo ya ghorofa moja ziligaa, kuwa madalali wanainadi kwa wapangaji wengine, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya wanaofuatilia maisha ya mlimbwende huyo ambaye ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz, kuwa huenda kashindwa kulipa kodi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Mama Mobeto alisema hata yeye kaiona nyumba hiyo ikinadiwa mtandaoni na madalali kama walivyoona watu wengine.

Amefafanua kwamba kwa kuwa wengi wanaijua nyumba ya Hamisa wamedhani ni yake lakini ukweli ni kwamba zinafanana tu kwani wanapoishi kuna nyumba tano za aina hiyo.

Katika nyumba hizo tano wapangaji wengi wanaokuja kuishi hapa ni wazungu, ambao baadhi yao wanafanya kazi kwa mikataba hapa nchini hivyo wakimaliza huwa wanaondoka, na hivyo mmiliki wa hizo nyumba kuwapa kazi madalali kutafuta wapangaji wengine na ndicho kilichoonekana mtandaoni, lakini ukweli nyumba hiyo sio tunayoishi sisi bado tupo sana na ikifika mahali tukitaka kuhama tutafanya hivyo,” alisema mama Mobeto.

Share.

About Author

Leave A Reply