Friday, August 23

LULU AMCHAGUA PIERRE, AMTOSA HAMISA

0


Staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema endapo ataambiwa amchague Pierre au Hamisa Mobeto katika kuigiza naye atamchagua Pierre.

Lulu ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha XXL kinachorushwa na kituo cha Clouds.

Awali mmoja wa waigizaji katika kpindi hicho, alimuuliza endapo kampuni ya kimataifa ya kuuza filamu na Neflix, aitakuja na kumpa nafasi ya kuchagua watu wawili kati ya Pierre na Hamisa kuigiza naye, atamchagua Pierre.

Alitaja moja ya sababu ya kumchagua kaka huyo kuwa ni kutokana na namna anavyochekeshesha na kwa kuwa yeye anapenda kucheka anadhani atafurahi zaidi.

“Yaani naona namna gani nitakavyokuwa nacheka tu wakati tukiwa location, Yesu wangu yaani nitacheka,” amesema Lulu.

Alipoulizwa kama ana mawasiliano na Hamisa, alisema hana na pia hawajawahi kuwa karibu hata huko nyuma.

Wakati suala la kuingilia mawasiliano yake na Majizo, alisema hawaezi kwa kuwa anajua ni watu wazima na wanachokifanya wanakijua na kuongeza kuwa wamejijemgea utaratibu wa kila mtu kuheshimu simu ya mwenzie.

Share.

About Author

Leave A Reply