Sunday, August 18

Kamanda wa Polisi Arusha Apata Ajali Mbaya ya Gari

0


Gari aliyokuwa amepanda Kamanda Charles Mkumbo


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali mbaya ya gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria kupasuka gurudumu ‘tairi’ ya nyuma na kupoteza muelekeo.

Taarifa hizo zilizothibitishwa na mlinzi wa Kamanda Mkumbo kwa njia ya simu ya RPC, amesema Mkumbo amepata ajali hiyo ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiitumia walikua watu watatu akiwemo msaidizi wake pamoja na dereva.

Kamanda Mkumbo amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha kwa ajili ya matibabu zaidi huku ikielezwa kuwa ameumia vibaya maeneo ya kichwani.

Chanzo: NipasheRead More

Share.

About Author

Comments are closed.