Saturday, August 24

Irene Amtupia Dongo Zito Wema Sepetu, Kisa Hiki Hapa

0Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.
Read More

Share.

About Author

Comments are closed.