Monday, August 26

DKT. PETER MITIMINGI AFUNGUKIA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

0


‘’Wataalam wanasema asilimia 90 halitokani na ugonjwa bali ni la kisaikolojia, wengi wanaopata tatizo hili hawajui tatizo lake ni nini, wengi wanadhani ni mambo ya kishirikina au kurogwa na kulipeleka tatizo hili sehemu zingine badala ya kutafuta suluhisho la kutafuta tiba ya msongo wa mawazo ambalo ndio chanzo kikubwa cha tatizo la nguvu za kiume’’ Alieleza Dkt. Peter Mitimingi.

Aidha alisema kuwa ulevi wa kupindukia ni chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume.

‘’Unapokunywa pombe kupita kiasi kuna sababisha sana tatizo hili, lakini pia tatizo jingine ni matumizi ya madawa kama madawa ya kisukari na figo, lakini aina za vyakula wanavyokula wanaume wengi, vyakula vyenye mafuta mengi, wali, chips na kuku wa kisasa ambao kw kiasi kikubwa wanakuzwa kwa madawa, wanaume wanatakiwa kula vyakula vya asili zaidi’’

Kuhusu swala la ndoa, Dkt. Peter Mitimingi amesema moja ya sheria za ndoa ni kwamba mchungaji au Sheikh akifungisha ndoa, huku akijua kuwa mwanaume ana tatizo la nguvu za kiume atafungwa jela miaka mitatu.

‘’Maana halisi ya ndoa ni tendo la ndoa’’ Alisema Dkt. Peter Mitimingi.

Share.

About Author

Leave A Reply