Thursday, August 22

Dereva Aliyemgonga Twiga, Mikumi Akimbia, Kupigwa Faini Mill. 34

0


Anasteria Ndaga, Afisa Uhifadhi Wanyama Pori Kanda Ya Mashariki akizungumza na mtandao wa Clouds FM amesema mnyama huyo aligongwa jana Mei 23, 2019, saa tano asubuhi, ambapo wanalishikilia gari hilo pamoja na msaidizi wa dereva wa gari hilo na amefikishwa katika kituo cha polisi.

‘’Dereva wa gari hilo amekimbia na hajapatikana hadi leo, tunawasiliana na mmiliki wa gari ili taratibu zingine zitafuata za kisheria’’ Alisema Anasteria Ndaga

Aidha amesema kuwa sheria za Uhifadhi za Taifa, zinasema mnyama kama Twiga anapogongwa faini ni U$ Dollar elfu 15, sawa na Mill. 34 za Kitanzania,  ameongeza kuwa zipo gharama zingine za uharibifu wa mazingira, na hawajampima kama Twiga huyo alikuwa mjamzito.

Share.

About Author

Leave A Reply