Saturday, August 17

Barakah The Prince: Nisingekuwa Msanii Ningekuwa Mwanajeshi

0
Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince amedai iwapo asingeingia katika fani hiyo basi angekuwa mwanajeshi.


Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Sometimes’ amekiambia kipindi cha Eight cha TVE kuna vitu visivyopungua vitano ambavyo vinamvutia kutoka kwa wanajeshi.

“Napenda mazoezi, napenda ule mchaka mchaka, napenda yale mavazi yao, napenda ile attitude yao, napenda ukarimu wao, yaani napenda the way walivyo,” ameema Baraka The Prince.

Barakah The Prince kwa sasa anafanya kazi zake chini ya label yake mpya Bana Music baada ya kuondoka RockStar4000 mwishoni mwa mwaka jana. Mwaka 2015 alishinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kama msanii bora anayechipukia.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.