Saturday, August 24

ATOA FIGO KUOKOA MAISHA YA MPENZI WAKE

0


ATOA FIGO KUOKOA MAISHA YA MPENZI WAKE – MWANAHARAKATI MZALENDO ™

New

Yanaitwa ‘MapenziMubashara’, kumwonyesha mtu mapenzi ya kweli sio tu kumwambia unampenda bali kuonyesha kwa vitendo.


Mwanaume mmoja aitwaye Aldo Cataldi (27) nchini Uingereza ameokoa maisha ya mpenzi wake, Geraldine Chingosho (22)  kwa kumpa figo yake moja.


Geraldine Chingosho alianza kusumbuliwa na figo muda mrefu hata kabla ya kukutana na Aldo Cataldi. Baada ya muda kwenye mahusiano yao wahudumu wa hospitali walimshauri Aldo Cataldi ya kwamba Geraldine atatakiwa kukaa hospitali hataweza tena kutoka na kuingia kwani alitakiwa kubadilishiwa figo.


Lakini Bwana Cataldi alibaki na mpenzi wake hospitalini na lilikuwa ni jambo zuri kwani vilipokuja vipimo juu ya mtu anayeweza kumwekea figo Gereldine ni vipimo vya Cataldi tu ndio vilionyesha kuendana na yeye ndiye aliyeruhusiwa kutoa figo kuokoa maisha ya Geraldine.

Na mara baada ya kupona Geraldine chingosho kutoka mji wa Lecester alisema ”Sikutegemea kama mpenzi wangu angeweza kutoa figo kwa ajili yangu na nimefurahi kuona figo zetu zinaendana”
Aliongeza kwa kusema kuwa “Aldo ameokoa maisha yangu ninachosubiri ni kuishi naye pamoja maisha yetu yote.

Share.

About Author

Leave A Reply