Tuesday, August 20

Amin Akwama Kuhusu Linah

0


Amin Akwama Kuhusu Linah – MWANAHARAKATI MZALENDO ™

New

STAA wa Bongo Fleva Amin Mwinyimkuu amefunguka juu ya madai ya kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Linah na kusisitiza wakati wa kusema ukweli ukifika ataweka wazi, lakini kwa sasa amewekeza zaidi kufanya naye kazi.

Amin na LinahAmin na Linah ambao waliwahi kuwa wapenzi na baadaye kuachana, hivi karibuni wameachia ngoma mpya inayojulikana kwa jina la ‘Nimenasa’, huku wengi wakiamini wawili hao wamerudiana baada ya kila mmoja kuachana na mpenzi wake wa zamani.


Amin alisema, kwa sasa hawezi kuzungumzia lolote kuhusu habari hizo na badala yake amesisitiza wakati wa kusema ukweli ukifika kila kitu kitajiweka wazi.


 “Unajua pamoja na watu kuzungumzia sana jambo hili, nadhani huu si wakati wa mimi kusema, mapenzi hayana siri, nadhani wakati wake ukifika kila kitu kitajulikana, mimi na Linah kwa sasa ni kazi tu, tunataka kufanya muziki wetu ukue zaidi kwa kuwa ndio kila kitu kwetu,” alisema Amin.

Share.

About Author

Leave A Reply