Wednesday, July 17

Arsenal yachapwa 2-0, Robben adaiwa kumtemea mate Sagna

0


Mchezo wa Ligi ya Mbaingwa barani Ulaya uliopigwa jana kati ya Arsenal ya England dhidi ya mabingwa watetezi, Bayern Munich ya Ujerumani katika dimba la Emirates jijini London, uligubikwa na kila aina ya vituko ikidaiwa Roben alimtemea mate Sagna  na kituko kingine ni kadi nyekundu ya mlinda mlango wa Arsenal Wojciech Szczesny ambaye anadaiwa pia kuonesha alama zisizofaa ambazo huenda akaadhibiwa na UEFA.
Pia sahau kuhusu Mesut Ozil na David Alaba kukosa penalti kwa kila timu, jambo kubwa lililoibuka sasa ni Roben kudaiwa kumtemea mate Sagna ambaye alikuwa amelala chini wakati wa mchezo huo.

Watu mbali mbali hasa mashabiki wa soka duniani kote ambao wanatumia mtandao wa mawasiliano ya kijamii wa Twitter wameeleza hisia zao baada ya kuiona video ambayo inamuonesha winga wa Bayern Munich Robben akiwa amemuinamia mlinzi wa Arsenal Bacary Sagna na kumtemea mate kwenye nywele.

Wengi wa walioiona video hiyo wamekuwa wakidai kuwa ni kweli Roben alimtemea mate Sagna huku wengine wakisema kuwa ni jasho lililomtoka na siyo mate. 
Toa manoni yako, je ni mate au jasho?Read More

Share.

About Author

Comments are closed.