Saturday, July 20

Vitu Hivi Saba Vitabadilisha Muonekano Wako

0


Leo na share vitu saba ambavyo ukivizingatia basi am sure utakuwa stylish

Article hii imeandikwa na Da Nicky wa bongocelebrity 

Kuna Tips kibao humu hope you will all learn something like i did

 

Hizi tips pia zinaweza kukusaidia sana wakati unaenda kwenye interviews au ukataka kujichanganya na group ambayo siku zote una  admire au kuwa mmoja wao, bila kubaguliwa kwasababu za maana kama Networking groups.   Unaweza tumia njia hizi kununua vitu vyako au vitu ulivyonavyo bila kuvunja bank na ukaonekana ni mmoja au zaidi wa yule anaenunua kwenye high ends stores (Maduka ya ghali/designers) kwa jinsi tu unavyozipangilia.

Kuna aina nyingi  za vitu ambavyo vinaweza kukusaidia kuonekana na muonekano wa kukubalika/kuheshimika;  lakini leo nitaongelea  kuhusu muonekano wa mavazi ambao waweza kubadilisha muonekano wako kwa jamii; ukaweza kupata nafasi za kuonana na watu wa maana ambao wanaweza kukusaidia au ku invest katika  ndoto zako. Kumbuka mavazi yako ni kitu cha kwanza mtu anakiona kabla hujafungua mdomo wako.

  1. Vaa nguo zitakazo kutosha vizuri. (Tailored) hakikisha nguo inakutosha, sio kubwa na wala haikubani sana, vaa nguo itakayoonyesha mwiili wako vizuri. Kama unaujua mwili wako,  kila mtu ana sehemu ya mwili wake ambao anaupenda zaidi ya nyingine. Tafuta nguo ambayo itang’arisha zaidi sehemu unayoipenda na itafunika au kuziba sehemu ambayo hautataka ionekane.Na kwa wote jaribu kutovaa nguo ambazo ni kubwa kuliko mwili wako itakufanya uonekana rough badala ya kuwa sharp. Chini ni mfano wa shati kwa mwanaume, jinsi ya kujua kama ni perfect fit, hii pia kwa wanamke unaweza kuangalia wakati unavaa blazers, shati au hata gauni.FullSizeRender 11
  2. Vaa viatu vilivyochongoka mbele, Flat au Heels. Hii kwa wanawake.  Mwanamke ambae anavaa viatu vya chini au cha kisigino ambavyo vimechongoka mbele na vazi lolote yeyote inaonekana expensive(Ghali); kuna kitu kuhusu viatu vilivyochongoka vinafanya mguu unanyooka na unapendezesha muonekano wa outfit nzima, . Viatu vyeusi au nude ni rangi zilizokuwa popular na vinaenda na kila outfit. Vinashauriwa kuwa ni moja ya aina za viatu jaribu kuwa navyo kabatini. Chini tumeonyesha jinsi viatu hivyo vinavyoweza valiwa na outfit tofauti.

    pointed shoes

  3. Vaa Statement Jewelry;  Statement jewelry naweza sema ni jewerly kubwa ambazo zinaonekana unapozivaa,  Fancy Jewelry  ina polish muonekano wa outifit wa aina yoyote, Hakuna Statement jewerly nzuri kama ambazo zinatengenezwa Africa. Kwa mfano Tanzania Enjipahi ni mzuri sana katika kutengeneza hizi statement jewelry, especially necklaces. Zaidi ya huyo naweza sema ukitembea tembea lazima utaona aina hizi za jewerly all over Africa. Tafuta chache uzipendazo na unazoweza ku afford. Kama ukivaa suruali nyeusi na blouse nyeupe ukiongeza na statement necklace, au hereni au bracelet, outfit yako instantly itaonekana glammed.

    Statement-jewerly-768x941

  4. Coordinate viatu na handbag(Mechisha viatu na begi) kufanya muonekano wako uwe polished, jaribu ku mechisha viatu vyako na handbag uliyobeba. Kama umevaa kiatu cheusi basi beba begi jeusi, na kama umevaa viatu vya brown then hakikisha unabeba handbag ya rangi ya brown(Hapa kidogo nitaomba sana uangalia matrial ya viatu vyako na handbag yako ili viendane, rangi ni muhimu, lakini materials lazima nazo ziendane). Lakini pia unaweza kutoka kidogo kuvaa viatu vyeusi na handbag ya nude, au  viatu vya rangi za  solid colours  kama pink, Red, na hata chuichui  vinaendeza na handbags ya rangi nyeusi. Chini ni mfano wa models walivyopangilia mguu na mkononi.(Muhimu hapa ni jinsi ya wewe kujisikia confortable na rangi)cordinate-shoes-and-bags-768x941

    Zaidi soma HUMU


Share.

About Author

Leave A Reply