Saturday, July 20

TBT :: STORY YA ANETH GERANA ISAYA DADA KIZIWI AMBAYE NI MSOMI NA MJASIRIAMALI PART 1

0


DAY 1 STORY
Anneth: Ninaitwa aneth gerana isaya nilizaliwa nasikia kama ninyi ndugu zangu lakini kwa bahati mbaya nikaumwa nikapata matatizo ambayo yalinipelekea kupoteza uwezo wangu wa kusikia ndio maana sasa mimi ni kiziwi lakini pamoja na Hali hiyo sikukubali kabisa kupoteza dira na Malengo yangu ya kusoma hadi chuo kikuu
Anneth: Kwanza kabisa namshukuru Mungu wa mbinguni maana ni kwa neema yake leo nipo hapa kuwapa ushuhuda huu kwa maana bila yeye nisingekuwa hapa leo nasema asante Mungu wangu wewe ni Ebenezer
Anneth: Pili namshukuru admin Yunus kwa kutambua dhamani yangu kwenu akaona heri aniletee huku mnisikie nilipoingia humu nilikuta watu kumi tu nikamwambia kama unataka nisimulie jitahidi ongeza watu wafike 50 kwa maana nataka ushuhuda wangu unoe vichwa vingi na kweli tangu jana anasaka watu kwa juhudi na maarifa hatimaye mmefika 50na zaidi hongera admin kwa juhudi hii group litafika mbali
Anneth: Nawashukuru wazazi wangu pamoja na mimi kupata matatizo lakini walinipeleka shule ya viziwi tabora ambapo nilisoma darasa LA kwanza hadi LA saba shule ilikuwa special kwa wanafunzi viziwi hivyo sikupata shida sana na nikafaulu kwa alama nzuri zilizoniwezesha kwenda shule ya sekondari ruvu iliyopo mikoani pwani
Anneth: Bahati mbaya si kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na form five badala yake nikapangiwa chuo cha ualimu sumbawanga…. Dhamira yangu ilikuwa ni kusoma form five halafu niende chuo sikutaka kabisa njia za mkato…. Nikafunga safari hadi wizara ya elimu nikawaambia wanipange shule yoyote ya form five wakasema haiwezekani kwa sababu hamna shule ya form five special kwa viziwi nikamwambia nipeni hivyo hivyo yakinishinda nitanyosha mikono narudi nyumbani.a33c4e80b017bab0e59f1d6bcc7bae50
Anneth: Nikasoma kwa juhudi sana bila kujali mazingira magumu hivyo nilipomaliza form four pale nikawa kiziw wa kwanza kufaulu kwa alama nzur tangu shule ianze kupokea wanafunzi viziwi
Anneth: Shule ya sekondari ruvu haikuwa maalum kama ilivyo tabora hivyo mazingira yalikuwa magumu kwangu mana tulichanganyika na wanafunzi wanaosikia mpaka nafika pale hakuna kiziwi aliyewahi kufaulu kwa alama za one two three zaidi ya four ya mwisho na zero hivyo tulikuwa kama wasindikizaji lakini mimi nikajisemea penye nia Pana njia japo mazingira magumu nitapambana mpaka kieleweke.

Anneth: Basi wakanipa barua ya kwenda iringa girl kusoma form five….. Nakumbuka siku naenda kuripot nilikuwa na shemeji yangu na nilienda nimechelewa na siku nafika ilikuwa jumamosi tukamkuta mwalimu wa zamu alipogundua sisikii hapo hapo akaanza kusema mmh huyo ataweza kusoma kweli???? Shule yenyewe hajawahi kupokea viziwi wala haina walimu maalum bora arudi tu nyumbani hapa anapoteza muda tu… Yaani shemeji aliponiambia huyo mwalimu alichosema nililia kwa uchungu nikamwambia shem basi turudi home akasema wewe baki tu ukishindwa ndo urudi nikakubalib1ef96701737c7a94afc3339fdba0482

Anneth: Basi nikawa nimepokelewa na kweli shule nzima nilikuwa kiziwi peke yangu tofauti na ruvu sekondari angalau kulikuwa na viziwi wachache… Pia no special teacher aise siku ya kwanza naingia darasani nilidata si mnajua walimu wa form five wengi wao wanapenda kufundisha huku mnaandika bila kuandika ubaoni hapo ndo nikaanza kukata tamaa siku ya pili sikurudi darasani ikapita wiki nzima siendi darasani maana nikajisemea nilijifanya ngangari sasa nimepatikana si bora ningeenda chuo cha ualimu duuu.

Anneth: Ndugu zangu mkiona Hali tete hivi mjue neema inakuja nakiri sikutakiwa kukata tamaa hivi lakini it was out of my ability yaani lakini all in all monitress wa darasa akapata habari kuwa siingii darasani akanifuata akaniambia twende kwa mkuu WA shule kutafuta msaada tunaenda mwee mkuu WA shule nikamuona anasema haloooo haloooo hapa iringa girl niongee kumbe anawapigia wizara ya elimu akawambia yule binti kiziwi mliyemleta yamemshinda sasa tufanyeje? Wakamjibu next week Kuna ugeni toka wizarani kuja iringa so wangepita kuniona tukawa tunawait to meet na hao vibosile.

Annet Kiziwi: Anneth: Basi siku ya siku ya siku maafisa WA wizara wakaja wakauliza nini tatizo nikaelezea ikiwa pamoja na kukosa mwalimu special anayejua sign language which is sped218daaeeb3e9db8fc7fd30e109b8f2ecial language for the deaf….. Wa kaniambia anet usikate tamaa wizara tunajua una mazingira magumu jitahidi hata upate four tutakufikiria uende advanced diploma kusema kweli maneno yao yaliniingia yananipa matumaini mpya na ari na moyo wa kugo ahead kabla ya hapo nilikuwa nakaa nyuma lakini baada ya hapo nikahamisha dawati nikawa mbele kabisa…. Nikaanza kumfundisha sign language friend yangu edith baada ya one month alikuwa fluency in sign language akageuka kuwa mkalimani wangu in classes and group discussion as well

Anneth: And true friend unamjua wakati wa matatizo… She will be there for you in all the way no matter what.

Anneth: Safi katika uanaharakati au mpambano jiamini thubutu…. Hakika si watu wote watauunga mkono lakini wapo wengine watakuunga mkono kwahiyo washikilie wale tu Watakuunga mkono na wale wasiokuunga wawe challenge kwako kama sehemu ya kufikia mafanikio kwa sababu siku zote huwezi kupata mafanikio bila kupitia challenges tofauti and challenges always makes u grown strong.

Anneth: Mhula wa kwanza nakumbuka nilishika Nafasi ya Nane kati ya wanafunzi sitini na Mhula uliofuata nikashika Nafasi ya Tatu!
Anneth: Na yeye alifaulu tulikuja kukutana naye udsm

Annet Kiziwi: Anneth: It gives me hope to looking forward….. Na nikakazana kadri ya uwezo wangu mpaka nitamaliza shule na division two two yangu mkononi pamoja na cheti cha ubora wa taaluma kwa heshima yangu niliwaomba wizara waanze kuleta viziwi form one kwani shule ilikuwa one hadi six wakakubali mpaka leo inapokea wanafunzi viziwi ikumbukwe kabla sijafika ilikuwa haipokei so am proud I opened a way for them
Anneth: Nitaenda hoster nikaanza kutafakari ikumbukwe friend yangu wa iringa girl yeye alijiunga udsm nikiwa second year so hakuwepo in my first year may be she could help me once again nikamkumbuka… I cry alone think what to do.7eedf2d10427eda42a1387972a37ba78

Anneth: Basi nikapata admission ya kwenda kusoma sociology aise baada ya kufika chuo siku ya kwanza naingia darasani si mnawajua maprofesa hawaandiki kabisa ubaoni nikastukia wenzangu wapo busy wanaandika notes huku profesa anafundisha kama vile mchungaji anavyohubir duu nitanyosha mkono nikasema nimadhinda nyuma kwa shida kabla sijakaa sawa nakutana na challenge hii tena aise I was very very disappointed

Anneth: Nikamwambia plz profesa help me akaniambia si nilikuambia hapa huwezi kusoma bora uende marekani nikamwambia kwa hiyo kila kiziwi atakayekuja hapa mtampeleka marekani? Kwanini msisaidie mimi ili kuwafungulia njia wengine? Akauliza sasa tutakusaidiaje? Nikawaambia ajirini mkalimani anisaidie kutafsiri darasani…. Seminar and group discussion akahema kwa nguvu akasema haya nenda tunalijadili

Anneth: Nikaa mwezi mzima siendi class a new friend of mine akanifuata akaniambia Anne hapa utadiscontinue yaani ndo nilikuwa nasikia about this nikamuuliza kudico ndo nini akanifafanulia kuwa ukifeli hapa no kuendelea na masomo yewiii nikatoka nduki huyo hadi kwa profesa maboko.

Anneth: Hao masista mnaowaona ni walimu wangu wa shule ya msingi viziwi tabora walifunga safari toka tabora kuja kuungana nami katika safari yangu ya ushindi na huyo dada mzungu ni kiziwi mwenzangu toka marekani kwangu mimi ilikuwa turufu ya ushindi
Annet Kiziwi: Anneth: Mpaka nimemaliza chuo mwaka 2009 baada yangu Kuna viziwi wawili, walinifuata wao walisomea education na walitumia wakaliman niliowaandalia mpaka sasa wapo wengine watatu so am proud again to open the door for them

Anneth: Nikamwambia plz profesa help me akaniambia si nilikuambia hapa huwezi kusoma bora uende marekani nikamwambia kwa hiyo kila kiziwi atakayekuja hapa mtampeleka marekani? Kwanini msisaidie mimi ili kuwafungulia njia wengine? Akauliza sasa tutakusaidiaje? Nikawaambia ajirini mkalimani anisaidie kutafsiri darasani…. Seminar and group discussion akahema kwa nguvu akasema haya nenda tunalijadili

Anneth: Tangu hapo nikawa naingia darasani bila matatizo yaani nikadhiriki kikazi life nilipofika second year chuo kikaongeza mkalimani mwingine nikawa nao wawili life at the University ikawa easy nikasoma hadi nitamaliza degree yangu kwa ushujaa

Share.

About Author

Leave A Reply